27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

MASHEIKH WALIOPOTEA ZANZIBAR WAPATIKANA


Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR   |   

MASHEIKH watano waliotekwa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha visiwani hapa, hatimaye wamepatikana.

Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Amir Haji Khamis Haji na wenzake wanne waliotoweka Februari 9, mwaka huu, waliachiwa juzi na kuungana na familia zao.

Akizungumza baada ya kuachiwa na watu hao, Amir Haji, alisema baada ya kukamatwa na watu hao, alifungwa kitambaa usoni na kupelekwa asikokujua na watu hao wasiojulikana.

“Binafsi siwajui hata waliofanya hivyo, lakini hadi leo hii (juzi) kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu milango ya asubuhi saa tano na nusu, naona nimeachiwa huru bila kuwa na madhara yoyote ikiwemo kuuawa.

“Na sasa niko nyumbani ni mzima, sikupata athari ya kupigwa na kitu chochote, kwahiyo nawaomba Waislamu wote waridhike na hilo, tuwe pamoja na waniombee dua mzee wao, hakuna kilichoharibika.

“Tuendelee na tuko pamoja na tuhifadhi mambo ya baadaye Inshallah. Sikuulizwa maswali yoyote, naona wao walikuwa wakifanya kazi yao, nasi kwa upande wa dini tunafanya pia.

“Kitu muhimu ni kuangalia masilahi ya baadaye na kuweka amani na hawa waliofanya haya nafikiri walikuwa wakifanya haya kwa ajili ya kuweka amani,” alisema Amir Haji.

Hata hivyo, alisema siku zote watahakikisha ….

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles