WASHIKILIWA NA POLISI KWA MAUAJI

0
1022

Na Pendo Fundisha, Mbeya

Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya, limefanikiwa kukamata silaha mbili ikiwemo Short Gun iliyokuwa ikimilikiwa na Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT, Itende mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema haya leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa katika tukio hilo watu watano wanashikiliwa kwa kukutwa na silaha hiyo pamoja na mauaji ya Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT, Chewe Willison yaliyotokea Februari 26, mwaka huu.

Kamanda Mpinga, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamid Shaban, Ibrahimu Mbilinyi, Stany Wema, Bahati Layland na Sambas Samson.

Aidha, amesema watuhumiwa hao walipohojiwa na askari wamesema silaha hiyo waliagizwa na mtu ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ‘dau’ la milioni tatu na kwamba anatafutwa na Polisi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here