25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

DK. ABBAS: NDEGE MPYA NNE ZA SERIKALI KUWASILI JULAI


Na SARAH MOSES-DODOMA  |  

SERIKALI imesema ifikapo Julai mwaka huu, ndege zote zilizoagizwa ikiwemo ya Boeing Dreamliner, zitakuwa zimewasili nchini.

Hayo yalisemwa jana mjini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kutokana na ujio wa ndege hizo, tayari ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vya kimataifa, kitaifa na kimkoa unaendelea kwa kasi.

“Kutakuwa na jumla ya ndege nne ikiwamo ya Boeing Dreamliner hivyo basi wale wote wazandiki na wanafiki ambao wamekuwa wakisemea vibaya wameshashindwa na hawana jipya”alisema Abbas.

Alisema viwanja vya ndege zaidi ya 10 ukarabati unaendelea katika mikoa mbalimbali ikiwamo  ya Kigoma, Tabora, Mwanza, Geita, Shinyanga, Sumbawanga, na Mtwara.

Vilevile alisema ujenzi wa Terminal III Dar es salaam uko zaidi ya asilimia 50 nakuongeza kuwa jengo la abiria uwanja wa kimataifa wa Songwe limefikia asilimia 57.

TANZANIA YANG’ARA

Wakati huo huo Dk. Abbas alisema Tanzania imezidi kung`ara baada yakupanda kwa nafasi 13 juu kidunia kutoka nafasi ya 216 hadi 203 katika jitihada za kupambana na rushwa.

Vilevile alisema Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Transparency International (Corruption Perception) inayoangalia hali ya rushwa na mapambano dhidi ya ufisadi.

Alisema ripoti hiyo ilitolewa February 21 mwaka 2017  ambapo mapambano na jitihada hizo anazifanya …

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles