25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki Afrika Kusini wamuwakia Beyonce

CAPE TOWN, AFRIKA KUSINI

MASHABIKI wa muziki nchini Afrika Kusini, wanaamini muziki wao unavuka boda huku wakitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kudai mwanamuziki nyota duniani Beyonce Knowles amakopi na kupesti video ya msanii wao Petite Noir.

Beyonce kwa sasa anatamba na albamu ya The Lion King, huku ndani kukiwa na wimbo Spirit ambao video yake inafananishwa na video ya msanii Petite, inayoitwa La Maison Noir, iliyoachiwa Oktoba 5, 2018.

Mashabiki hao wamedai hakuna sababu ya kumsifia Beyonce na video ya wimbo wake wa Spirit kwa kuwa msanii wao Noir ndiyo wa kwanza kuachia video yenye maudhui hayo.

“Hii inaonyesha muziki wa Afrika unavuka mipaka, Beyonce wala hasistahili kupewa sifa lakini Noir anastahili kwa kuwa yeye ni msanii wa kwanza kuachia video tangu mwaka jana, Beyonce atakuwa amefanya kosa kukopi,” alisema mmoja ya mashabiki wa muziki Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles