Korea Kaskazini yafyatua makombora tena

0
698

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

JESHI la Korea Kusini, limesema Korea Kaskazini limefyatua tena makombora mawili jana na kwamba makombora hayo ambayo hayajatambuliwa ni ya aina gani yalianguka baharini.

Hayo ni majaribio ya tatu ya makombora ndani ya wiki moja ambayo yamefanywa na Korea Kaskazini.

Hatua ya Korea Kaskazini kuzidisha majaribio yake ya makombora, inatizamwa kama mbinu yake ya kuongeza shinikizo kwa Korea Kusini na Marekani dhidi ya kasi yake ya polepole kuhusu mazungumzo ya silaha za nyuklia.

Julai 25, Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya kombora lake ambalo ilisema ni vigumu kulidhitibi.

Korea Kaskazini pia ilisema majaribio yake ni onyo kwa Korea Kusini kuhusu mpango wake wa kufanya zoezi  pamoja na la kijeshi na Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here