28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

MARIAH CAREY AANZA ZIARA YA KRISMASI

NEW YORK, MARAKENI


NYOTA wa muziki nchini Marekani, Mariah Carey, amesema hiki ndicho kipindi chake cha kutamba na wimbo wake wa ‘All I Want For Christmas Is You Tour’, mara baada ya kuanza ziara ya wiki mbili.

Msanii huyo wa muziki wa RnB, alifanikiwa kufanya vizuri katika albamu yake ya nne baada ya kuachia wimbo huo Novemba 1, mwaka 1994, ambapo aliutunga kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi.

Mariah ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuwapa habari mashabiki wake kuwa tayari ameanza ziara kwa ajili ya sikukuu hiyo na anatarajia kufanya vizuri na wimbo huo.

“Naweza kusema huu ndio mwezi wangu, ninaamini wimbo wangu wa ‘All I Want For Christmas Is You Tour’ huu wakati wake, nimeamua kufanya ziara ya wiki mbili kwa ajili ya kutamba na wimbo huo hadi siku ya Krismasi, hivyo mashabiki wangu naomba tuwe pamoja,” alisema Mariah.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles