24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

FAMILIA YA BIEBER YAMTAKA SELENA

NEW YORK, MAREKANI


KWA mujibu wa mtandao wa E! News, familia ya nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber, imesema ipo tayari kumpokea mpenzi wa zamani wa msanii huyo, Selena Gomez.

Wazazi wa msanii huyo, Mallette na Jeremy Bieber, wamesema watakuwa na furaha zaidi endapo Selena atakubali kurudiana na mtoto wao.

Wazazi hao wamekuwa wakijaribu kumfanya mtoto wao aonekane kuwa mtu wa dini ili awe na maadili mema na kumwekea mazingira mazuri ya kukubalika na mrembo huyo.

Mwezi uliopita, Bieber na Selena, walikuwa wanaonekana mara kwa mara wakiwa pamoja na kuenea taarifa kwamba wawili hao tayari wamemaliza tofauti zao na sasa wapo kwenye uhusiano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles