32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yarekodi kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira

WASHINGTON, MAREKANI

MAREKANI imerikodi kiwango kibaya kabisa cha kupotea kwa nafasi za ajira kutokana na athari za virusi vya corona wakati Ulaya ikiandamwa na kuongozeka kwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo.

Kiasi nafasi za kazi milioni 20.5 zimepotea ndani ya mwezi April huku ukosefu wa ajira ukipanda hadi asilimia 14.7, ambacho ni kiwango cha juu zaidi tangu mdodoro wa uchumi wa miaka ya 1930.

Taifa hilo lenye uchumi mkubwa duniani limekabiliwa na kishindo cha janga la virusi vya corona ambalo tayari limesababisha vifo vya watu 75,000 nchini humo pamoja na maambukizi yanayofikia milioni 1.2

Akitilia maanani uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba, rais Donald Trump ameahidi kuifungua tena nchi hiyo na idadi kubwa ya magavana wa majimbo mbalimbali nchini Marekani wameruhusu shughuli za biashara kuanza tena japo kwa hali ya tahadhari.

Rais Trump amepuuza wasiwasi unaotokana na takwimu hizo akisema ishara za hivi karibuni za kuimarika kwa masoko ya mitaji ni uthibitisho kuwa mambo yatatengamaa katika kipindi kifupi kinachokuja.

“Tutakuwa na mwaka mzuri, hapo mwakani na nadhani utatujia kama upepo ” amesema Trump wakati wa mkutano wake na waandishi habari mjini Washington.

Matumaini yake yanakuja wakati virusi vya corona vikiripotiwa kusambaa ndani ya ikulu ya White House baada ya msemaji wa makamu wa rais Mike Pence kugundulika kuwa ameambukizwa.

Katika taifa jirani la Canada, kiasi nafasi za kazi milioni 3 zimepotea na kusababisha kiwango cha ukosefu wa ajira kupanda hadi asilimia 13.1 , siku mbili tangu Umoja wa Ulaya ulipobashiri kutokea mdodoro mkubwa wa uchumi kwenye kanda hiyo.

Matumaini yamekuwa yakiongezeka kuwa kilele cha kadhia hiyo ya ulimwengu ambayo imewauwa zaidi ya watu 270,000.

Lakini baada ya wiki kadhaa za vizuizi vikali duniani kuzuia kusambaa virusi vya corona , matokeo ya maumivu yameanza kuonekana katika eneo la uchumi ambapo sasa dunia inaonekana kukabiliwa na mdodoro mbaya kabisa katika kipindi cha karibu nusu karne.

Katika hatua nyingine mawaziri wa Fedha wa mataifa ya kanda ya sarafu ya Euro wameidhinisha kiasi dola bilioni 260 kuyasaidia mataifa ya Ulaya kufidia gharama kubwa za kupambana na mlipuko wa virusi vya corona.

Mpango huo utaosimamiwa na mfuko wa uokozi wa kanda ya sarafu ya Euro ni hatua kubwa ya kwanza katika juhudi za Umoja wa Ulaya kuupiga jeki uchumi ambao makadirio yanaonesha utasinyaa kwa asilimia 7.7 mwaka 2020.

Chini ya makubaliano hayo kila nchi mwanachama wa umoja wa sarafu ya Euro itaweza kuchukua mkopo wa riba nafuu huku mataifa yaliyoathriwa zaidi kama Italia na Uhispania yatapatiwa kiwango kikubwa cha fedha za uokozi.

Wakati huo huo Marekani  imeimarisha  sheria ya viza za kusafiria kwa wanahabari wa China

Marekani imetangaza sheria mpya ya kutilia mkazo mwongozo wa viza za kusafiria kwa wanahabari wa China na kusema hatua hiyo inatokana na jinsi wanahabari wa Marekani nchini China wanavyochukuliwa.

hili linakuwa ni suala jipya linaloibuka huku kukiwa na hofu kati ya mataifa hayo mawili kuhusiana na janga la kimataifa la virusi vya corona.

Marekani na China zimehusika katika misururu ya hatua za kulipiza kisasi zinazowahusisha wanahabari katika miezi ya hivi karibuni.

Mnamo mwezi Machi, China iliwafukuza  wanahabari wa Marekani kutoka kwenye kampuni tatu za magazeti, mwezi mmoja baada ya Marekani kusema itaanza kuvichukulia vyombo vitano vya habari vya serikali ya China sawa na balozi za kigeni.

Sheria hiyo itakayoanza kutekelezwa siku ya Jumatatu, itaweka muda wa visa za wanahabari wa China kuwa siku 90 huku kukiwa na chaguo la kuongeza muda huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles