28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

WHO yatayarisha programu ya kujipima corona kwa simu

GENEVA, USWISI

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema linapanga kuzindua programu ya simu ya mkononi itakayowawezesha watu kujipima iwapo wameambukizwa virusi vya corona.

WHO imekuja na program hiyo katika wakati ambao pia Marekani imekwishaidhinisha kipimo kipya kinachoweza kutumiwa nyumbani kwa kupima mate  na kubaini ugonjwa wa COVID-19.

 Kwa mujibu wa WHO, program hiyo mbali na kuwawezesha watu kutoka nchi zenye raslimali duni kujipima iwapo wamepata maambukizo ya virusi vya corona pia itakuwa msaada mkubwa kwao kwani wengi wao si rahisi kupata kipimo hicho kwa haraka kama yalivyo mataifa mengine makubwa duniani. 

Ofisa mkuu wa mawasiliano katika shirika hilo, Bernardo Mariano, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa WHO pia inazingatia uwezekano wa kutumia kifaa cha kufuatilia watu walioambukizwa kwa kutumia mfumo wa Bluetooth.

Akizungumzia kuhusu Programu hiyo na jinsi itakavyokuwa inafanya kazi, Mariano amesema kuwa programu hiyo itawauliza watu kuhusu dalili walizonazo na kutoa mwongozo kuhusu iwapo wana ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Maelezo mengine, kama vile jinsi ya kufanyiwa uchunguzi, yatawekwa kulingana na nchi ya mtumiaji wa programu hiyo.

Kupitia mahojiano kwa njia ya simu, Mariano amesema kuwa japokuwa shirika hilo la Afya Duniani litawezesha kupatikana kwa programu hiyo katika mtandao kote ulimwenguni, serikali yoyote duniani inaweza kutumia teknolojia hiyo na kuongeza miundo yake kutengeneza aina ya programu yake katika mtandao.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles