25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI, URUSI ‘VINARA’ BIASHARA YA SILAHA

STOCKHOLM, SWEDEN


MAREKANI na Urusi zinatajwa kuwa vinara wa kuuza silaha kwa zaidi ya nusu ya biashara yote duniani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana na Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Amani na Udhibiti wa Silaha (SIPRI) kuna ongezeko kubwa la biashara ya silaha kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu kumalizika kwa vita baridi.

Ongezeko hilo limechangiwa zaidi na kuongezeka kwa mahitaji yatokanayo na mzozo wa Mashariki ya Kati na Asia.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo yenye makao yake mjini hapa, kipindi cha mwaka 2012 na 2016, uagizaji wa silaha katika nchi za Asia na zilizozungukwa na Bahari ya Pasifiki maarufu kama mataifa ya Ocean ilifikia asilimia 43 ya biashara ya silaha duniani.

Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 7.7 ikilinganishwa na kipindi cha kati ya mwaka 2007 na 2011.

Mgawanyo wa uingizwaji wa silaha kimataifa katika mataifa ya Asia na Oceania ulipanda kati ya mwaka 2007 na 2011, huku mgawanyo katika nchi za Mashariki ya Kati na Ghuba ukipanda kutoka asilimia 17 hadi 29, mbele zaidi ya Ulaya, kwa asilimia 11, Amerika kwa asilimia 8.6 na Afrika kwa asilimia 8.1.

SIPRI imesema, biashara ya silaha kimataifa ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita imefikia rekodi ya juu zaidi tangu mwaka 1950.

Saudi Arabia, ilikuwa ya pili katika biashara ya uingizaji silaha, ikiwa nyuma ya India, tofauti na China ambayo bado haitengenezi silaha kwa kiwango cha kitaifa.

Marekani inasalia kuwa nchi inayoongoza kwa uuzaji wa silaha kwa asilimia 33, mbele ya Urusi yenye asilimia 23, China ina asilimia 6.2 na Ufaransa asilimia 6.0 huku Ujerumani ikifikia asilimia 5.6.

Mataifa haya matano yanafanya asilimia 75 ya mauzo ya nje ya silaha zote nzito duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles