25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

RAIS UHURU AONGOZA KURA YA MAONI KENYA

NAIROBI, KENYA


IWAPO chaguzi zingefanyika leo, asilimia 47 ya Wakenya wangempigia kura Rais Uhuru Kenyatta huku mpinzani wake Kiongozi wa Muungano wa Cord, Raila Odinga akitarajia kupata asilimia 30, kura za maoni zilizoendeshwa na kampuni ya Ipsos zimeonesha.

Asilimia sita ya Wakenya wangempigia kura kiongozi wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, na asilimia tatu Kiongozi wa Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi.

Ipsos jana ilitoa toleo lake la tano la kura ya maoni iliyofanyika kati ya Januari 9 na 26 mwaka huu.

Mchakato huo pia ulionesha kuwa asilimia 49 ya Wakenya inamtaka Odinga abaki katika siasa za ushindani na kuwania urais katika uchaguzi wa Agosti 8 kulinganisha na asilimia 35 iliyokuwa Juni 2016.

Ni asilimia 25 tu iliyotaka kiongozi huyo wa Cord astaafu huku asilimia 22 ikimtaka abakie katika siasa za ushindani lakini asishiriki uchaguzi wa Agosti 8.

Kwa kulinganisha uungwaji mkono wa maeneo unaonesha kuwa magharibi mwa Kenya ni eneo lenye ushindani zaidi kisiasa baina ya viongozi hao wawili, ambapo 36 wanamuunga mkono Odinga na 24 Rais Kenyatta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles