28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

MAREHEMU AWEKWA KWENYE PICHA ZA HARUSI ZA DADA YAKE

WAKATI kaka wa Catherine Carter alipofariki dunia katika ajali  wiki chache tu kabla ya ndoa yake, dada mtu aliumia vibaya mno kuona atamkosa wakati wa siku yake ya kihistoria aliyokuwa akiisubiri kwa hamu kubwa.

Lakini shukrani kwa mtaalamu wa picha, matakwa na ndoto yake isiyo ya kawaida ya kuona mdogo wake huyo akisimama kando yake katika picha ya familia ikatimia.

Mama huyo wa nyumbani alionana na mtaalamu huyo, Rachel Duncan kumuomba amfanyie maarifa ili picha ya harusi yake na John Flower imhusishe na marehemu kaka yake huyo, Shaun Carter.

Shaun (29), alifariki kwenye ajali Mei mwaka jana miezi miwili tu kabla ya ndoa ya dada yake.

Shaun inasemekana alikufa baada ya majereha ya kichwa na shambulio la moyo wakati alipoangukiwa na tingatinga katika eneo lililokuwa likifanyika ujenzi huko Cirencester, Gloucestershire nchini Uingereza.

Katika picha moja, Catherine anaonekana akiwa na mama na baba yake wa kambo na picha ambayo haijakolea sana ya nduguye huyo anayeoneakana kuweka mikono yake kwenye bega la Catherine.

Picha nyingine inamuonesha marehemu huyo akionekana mithili ya mzuka akiwa amemshika dada yake katika mkono wa kushoto.

Catherine anasema: “Ni mwujiza kumuona kwenye picha zangu za harusi, sikuweza kujizuia kutokwa na machozi.”

Inamaanisha mengi kuwa naye katika picha hizi, akiwa amesimama nasi. Nimezitundika katika sebule yangu kwa sasa.

Catherine aliolewa na Flower katika Kanisa la St Paul, Chippenham.

Rachel ambaye anachaji pauni 25 sawa na Sh 75,000 kwa kila taswira akiwa Ofisa wa Kampuni ya Jelly Penguin Graphics iliyounda picha hizo, anasema ombi la Catherine lilimgusa sana.

‘Aliniomba kumuongeza kaka yake katika piocha zake za harusi mna nilidhani naweza kumsaidia.

“Nilimpa onyo kwamba nitazianika picha hizo na kumuuliza iwapo yupo tayari, akalia. Kamwe sikujua kwa kiasi gani ilimpendeza Catherine.

“Tangu picha hizo ziwekwe kwenye Facebook, zimependwa na zaidi ya watu 2,000 na mamia ya watu wamezitolea maoni, anasema.”

Wengi wanasema wao pia wangependa picha zao wenyewe ziongezwe wapendwa wao ambao walifariki dunia. Kitu ambacho kimefanikiwa kupromoti biashara ya Flower.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles