25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Marais 10 wahudhuria mkutano Sadc

NORA DAMIAN – DAR ES SALAAM

MARAIS 10 kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamehudhuria mkutano wa 39 wa jumuiya hiyo ulioanza jana.

Marais hao na nchi wanakotoka kwenye mabano ni Dk. Hage Geingob (Namibia), Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Danny Faure (Shelisheli), Edgar Lungu (Zambia), Joao Lorenco (Angola) na Felix Tshisekedi (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo).

Wengine ni Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe), Azali Assoumani (Comoro), Andry Rajoelina (Madagascar) na Filipe Nyusi (Msumbiji).

Mbali ya marais hao nchi nyingine ziliwakilishwa na makamu wa rais, mawaziri wakuu na mawaziri wa mambo ya nje ambapo Malawi iliwakilishwa na Makamu wa Rais, Saulos Chilima, Lesotho iliwakilishwa na Waziri Mkuu, Dk. Motsoahae Thabane.

Nchi nyingine ni Mauritius iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Nandi Botha, Eswatini iliwakilishwa na Waziri Mkuu, Ambrose Dlamini, Botswana iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Pelomoni Venson-Moitoi.

Viongozi hao waliwasili nchini kwa nyakati tofauti tangu Jumatano wiki hii na kupokelewa na wenyeji wao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Rais wa Afrika Kusini, Ramaphosa aliwasili nchini tangu Jumatano usiku na kufanya ziara ya kikazi ambayo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kuzuru makaburi ya wapigania uhuru wa nchi hiyo yaliyopo eneo la Mazimbu mkoani Morogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles