23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Maradhi muhimu kwa mwanamke kuyagundua mapema

why-you-should-go-to-your-postpartum-check-up-800x500Na JOACHIM MABULA,

JINSI maisha ya leo yalivyo na pilika pilika, kupata muda wa kumuona daktari kama ukiwa hauumwi huwa ni vigumu, lakini ni muhimu kutosahau afya yako. Mwili wa binadamu ni kama mashine tata inayofanya kazi nyingi na ili ufanye kazi vizuri unahitaji matunzo na uchunguzi wa mara kwa mara kuhakikisha ubora wake. Uchunguzi wa afya kwa kawaida ni muhimu kwa wanawake wote bila kuzingatia umri hata kama huna dalili za ugonjwa wowote.

Uchunguzi kamili wa afya ya mwanamke inahusisha uchunguzi wa mwili kiujumla, magonjwa ya moyo, kiwango cha cholesterol, kisukari, utendaji wa viungo vikubwa vya mwili, Osteoporosisi (aina ya kusinyaa kwa mifupa ya sehemu moja au mifupa yote miwili ambapo tishu ya mfupa hupotea lakini bila ya kuathiri muundo wa mfupa mzima) na saratani za aina mbalimbali  hasa zilizozoeleka mfano saratani ya ini, utumbo mpana na shingo ya kizazi.

Daktari huoanisha maelezo unayotoa toka kwenye dalili unazohisi, historia yako ya nyuma kiafya, uchunguzi wa mwili mzima na mwisho kufanyiwa vipimo ili kugungua magonjwa/maradhi au hatari ya kupatwa na magonjwa/maradhi. Vipimo na uchunguzi unaopaswa kufanyiwa unategemea umri, historia ya familia kiafya, maisha anayoishi mteja/mgonjwa; mfano anachokula, shughuli anazofanya na kama anatumia bidhaa za tumbaku kama sigara na kama anatumia pombe.

Wakati wa kuchunguza afya ya mwanamke, daktari anaweza kumwomba mwananamke afunue baadhi ya maungo yake au kuvua nguo kabisa ili kufanya uchunguzi vizuri. Vitu vinavyoweza kufanyika ni pamoja na kuchukua sampuli kwa pamba kwenye uke au seviksi, sampuli ya mkojo, sampuli ya damu na kuchunguza sehemu za nje za utupu wa mwanamke.

Kuna magonjwa ambayo ni  muhimu kwa mwanamke kufanyiwa uchunguzi mapema. Maradhi hayo ni pamoja na:

Kupima kiwango cha ‘cholesterol’

Maisha ya anasa tunayoishi siku hizi pamoja na vyakula tunavyokula na mafuta tunayopikia vyakula vyetu yanatuweka katika hatari ya kupanda kiwango cha cholesterol kwenye damu yetu kinachoweza kusababisha magonjwa ya moyo. Hivyo, ni muhimu kupima kiwango cha cholesterol kama kinastahili au kimezidi.

Magonjwa ya zinaa kama Klamidia

Klamidia ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria waitwao klamidia. Wanawake wanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huu kila mwaka tangu walipo balehe.

Virusi vya Ukimwi (VVU)

Ni muhimu kupima VVU ikiwa unajihusisha na vitendo vya ngono na ukiwa mjamzito ni lazima kupima ili kama una maambukizi uanze matibabu ya kumkinga mtoto aliye tumboni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles