24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Utafiti: Vinywaji vya kuongeza nguvu husababisha matatizo ya ini

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

UNYWAJI wa mara kwa mara wa vinywaji vinavyoongeza nguvu mwilini ‘energy drinks’ unasababisha ini kushindwa kufanya kazi (acute hepatitis).

Kwa mujibu wa ripoti za magonjwa zilizochapishwa kwenye  jarida la BMJ Case Reports Novemba Mosi mwaka huu, mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 50 amepata tatizo hilo baada ya kunywa ‘energy drinks’ mara kwa mara kwa muda wa wiki tatu.

Matatizo ya ini husababishwa na utumiaji wa dawa mara kwa mara pamoja na vidonge vya lishe hususani vya vitamin na wakati mwingine husababisha ini kufa kabisa.

Mwanamume huyo alimweleza daktari kuwa alikuwa anaumwa kwa wiki mbili akisumbuliwa na maumivu ya tumbo, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika.

Daktari aliyekuwa akimtibu aliandika katika jarida hilo kuwa awali mwanamume huyo alifikiri anaumwa mafua hadi aliposhtuka baada ya kuona anakojoa mkojo mweusi na ngozi ikiwa ya manjano.

Timu ya madaktari iliyokuwa ikiongozwa na Dk.  Jennifer Harb, mtaalamu wa ngozi na magonjwa yake wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Florida walifanya utafiti kuhusu uhusiano wa matatizo ya ini na unywaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu.

Madaktari hao waligundua kuwa mwanamume huyo hakuwa amepata aina yoyote ya matibabu wala kunywa dawa ila alikiri kuwa amekuwa akinywa chupa nne hadi tano kwa siku za vinywaji hivyo kwa muda wa wiki tatu.

Wakati wa vipimo waligundua kwamba maumivu ya tumbo ya mtu huyo yalikuwa yanatoka karibu kabisa na ini.

Madaktari walifanya vipimo zaidi ikiwamo kupima damu na majimaji ya ini ndipo walipogundua kuwa ini lake limepata matatizo. Pia mtu huyo aligundulika kuwa na homa sugu ya ini (hepatitis C).

Iligundulika kuwa vinywaji alivyokunywa vilikuwa na wingi wa vitamin B3 vikiwa na miligramu 40 ikiwa ni zaidi ya miligramu 20 zinazoshauriwa kwa siku.

Kwa sababu alikuwa anakunywa  chupa nne hadi tano kwa siku, madaktari hao wameandika alikuwa anakunywa  160 gm hadi 200 mg kwa siku.

Utafiti wa awali unaonyesha kuwa kula zaidi ya 500 mg za vitamin B3 kwa siku kunasabaisha sumu katika ini.

Madaktari hao wanasema kwa sabau alikuwa anakunywa kiasi cha 500 mg, atakuwa ameathirika kwa mlundikano wa vitamin hiyo kwa siku alizokuwa anakunywa vinywaji hivyo.

Kisa hicho kinafanana na kisa kilichoripotiwa katika jarida la ripoti za magonjwa la mwaka 2011 ambapo mwanamke mmoja aliripotiwa kupata matatizo ya ini baada ya kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu kwa wiki mbili.

Iliripotiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa anakunywa 300 mg za vitamin B3 kwa siku kwa kunywa vinywaji hivyo.

Madaktari hao wanasema kuna uwezekano kwamba vitu vingine vilivyopo kwenye vinywaji hivyo vilisababisha baadhi ya dalili licha ya kwamba hakuna taarifa za kutosha za kudhibitisha hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles