NA ZAINAB IDDY
KIUNGO wa Yanga, Mapinduzi Balama, amepewa programu maalumu ya mazoezi ili kurejesha mwili wake katika hali ya kiuchezaji kabla ya kuanza kutumika kwenye mechi mbalimbali.
Balama alipata majeraha la enka akiwa kwenye majukumu ya timu hiyo msimu uliopita kiasi cha kukosa michezo iliyokuwa imesalia kabla ya msimu kumalizika, sambamba na michezo yote
mitano ya msimu huu.
Doktari wa Yanga, Shecky Mngazija aliliambia MTANZANIA jana kuwa, nyota huyo aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Alliance ya Mwanza, kwa sasa yuko kambini na wachezaji wengine wa kikosi chao, ingawa amepewa programu maalum ya mazoezi kila siku, ili kuhakikisha anapona haraka.
“Kwa sasa anaendelea vizuri na ndio sababu ya kumtaka awe pamoja na wachezaji wenzake kambini,kwa ajili ya uangalizi mzuri.
“Kulingana na maendeleo yake, kila siku anatakiwa kukanyanga mchanga kwa nguvu mguu ule uliopata shida kwa muda wa nusu saa, mara tatu kwa siku,lakini pia anapokuwa amekaa tunamlazimisha kuutikisa kila mara,hii yote ni kuepusha mguu kukakamaa kitu ambacho ni hatari zaidi kwake.
“Kwa kufanya hivyo kutamchukua muda mfupi kupona kabisa na kuendelea na majukumu yake, japo siwezi kusema itachukua muda gani kwa sababu kila binadamu ana’nature'(asili)ya mwili wake unapopokea matibabu tofauti na mwingine,”alisema Mngazija.