24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mapigano yaua wanajeshi 150 Sudan Kusini

Riek Machar
Riek Machar

JUBA, SUDAN KUSINI

WANAJESHI 150 kutoka makundi yanayohasimiana wameuawa katika mapigano yanayoendelea mjini hapa na kuzusha wasi wasi wa kuvurugika kwa makubaliano ya amani.

Milio ya risasi, maguruneti na mizinga ilisikika tangu Ijumaa na kuendelea hadi jana katika maeneo ikiwamo karibu na Ikulu ambako Rais Salva Kiiri alikuwa akikutana kwa mazungumzo na makamu wake Riek Machar.

Viongozi hao wote wawili, ambao huo nyuma walikuwa mahasimu wamesema hawajui sababu ya mapigano hayo na wametoa wito wa utulivu.

Chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mafunzo mjini hapa, ambayo ni Hospitali Kuu ya Serikali kimepokea zaidi ya maiti 90 za askari na raia.

Kwa mujibu wa daktari mmoja katika hospitali hiyo, ambaye amekataa kutajwa, nyingi ya maiti zilikuwa za wanaume.

Msemaji wa Machar, James Gatdet amevilaumu vikosi vya usalama vya Kiir kwa kuzuka kwa mapigano hayo baada ya kuwashambulia walinzi wa makamu wa rais.

Aidha Gatijach Deng msemaji wa Kitengo cha Jeshi katika kundi la Machar amesema mapigano hayo yalitokea karibu na Ikulu na katika kambi za kijeshi.

Deng amesema asubuhi ya juzi walikusanya maiti 35 kutoka upande wa kundi la (SPL-IO) la Machar na 80 kutoka vikosi vya serikali.

Amesema idadi ya vifo itaöngezeka kwa upande wa kundi la Machar kutokana na uwepo wa majeruhi wengi mahututi.

Taifa hilo changa barani Afrika linaibuka kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza Desemba 2013 baada ya Kiir kumtimua Machar kutoka umakamu wa rais.

Vita hivyo vilipiganwa zaidi kwa misingi ya kikabila, ambapo Kiir alikuwa akiungwa mkono na kabila lake la Dinka na Machar akiungwa mkono na kabila lake la Nuer.

Makubaliano ya amani yaliyofikiwa Agosti mwaka jana yalikomesha vita hivyo lakini Kiir na Machar bado hakuweza kuunganisha vikosi vyao katika kipengele muhimu katika makubaliano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles