Mwili wa Elizabeth Mayemba kuagwa leo

Elizabeth Mayemba
Elizabeth Mayemba
Elizabeth Mayemba

NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

MWILI wa aliyekuwa Kaimu Mhariri wa Michezo wa gazeti la Majira, Elizabeth Mayemba aliyefariki dunia juzi, unatarajiwa kuagwa leo na kuzikwa kesho mkoani Morogoro katika makaburi ya Kola.

Eliza alikutwa na umauti juzi saa mbili usiku wakati akiwa njiani kukimbizwa katika Hospitali ya Amana Dar es Salaam baada ya kujisikia vibaya na kuanguka ghafla nyumbani kwake Tabata Kisukuru.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na uongozi wa Kampuni ya Business Times Limited inayozalisha magazeti ya Business Times, Majira na Spoti Starehe, mwili wa marehemu utaagwa saa 5:00 asubuhi nyumbani kwake leo baada ya misa na kusafirishwa kwenda Morogoro kwa mazishi.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wakati wa uhai wake, marehemu alifanya kazi zake na majukumu yote bila ya kuonesha dalili za kuumwa.

Ilieleza kuwa kampuni imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Elizabeth ambaye mchango wake ulikuwa mkubwa zaidi na hasa ulivyoonekana kwa kila mtu.

Marehemu ameacha mume na watoto watatu wa kiume, Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here