26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Obama akatiza ziara Poland

RAIS Barack Obama
RAIS Barack Obama

DALLAS, MAREKANI

RAIS Barack Obama alitarajia kukatiza ziara yake nchini Poland jana anakohudhuria kikao cha Jumuiya ya Kujihami ya Magharibi (NATO) kufuatia mauaji ya maafisa watano wa Polisi.

Mauaji hayo yalifanywa na afisa wa jeshi mwenye asili ya Kiafrika dhidi ya maafisa watano wa polisi Wazungu mjini Dallas katika kile kinachoonekana kuzorota kwa uhusiano baina ya Wazungu na raia weusi wa Marekani.

Polisi walikuta vifaa vya kutengeneza mabomu na silaha nyingi nyumbani kwa afisa huyo wa jeshi aliyetambuliwa kama Michah Johnson mwenye umri wa miaka 25.

Johnson ambaye ni mkazi wa hapa aliwaua maafisa hao watano kabla ya kupigwa risasi wakati wa makabiliano makali.

Huku Ikulu ya Marekani ikikanusha kuwa Johnson alikuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi, mtandao wake wa Facebook ulionyesha alikuwa katika kikundi cha wanaharakati wanaopinga ubaguzi dhidi ya weusi Marekani.

Akitambulika kama ‘mshambuliaji aliyejitoa mhanga’ na ambaye hakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu, Johnson aliwaeleza waliokuwa karibu naye kabla ya kuuawa kuwa alitaka kuwaua maofisa Wazungu wa polisi kulipiza kisasi cha mauaji ya Wamarekani wawili weusi wiki iliyopita.

Mashambulizi hayo yalisababisha vurugu kubwa wiki iliyopita katika jimbo la Texas wakati wa maandamano ya amani ya kupinga ukatili wa polisi.

Shambulizi hilo lilitokea wakati wa kipindi cha kurejesha uhusiano kutokana na makabiliano kati ya Waafrika na Wamarekani.

Akihutubia umati kwa heshima ya waliouawa Meya wa Dallas, Mike Rawlings aliwasihi Wamarekani watulie na kudumisha amani wakati huu wa kurejesha uhusiano na na kulaani ubaguzi uliokithiri.

“Kamwe hatutaona haya kusema jiji hili na taifa hili linakumbwa na ubaguzi wa rangi,” Meya huyo aliuambia mkutano huo.

Rawlings alikariri hotuba ya Rais Obama kuwa nchi inajidhatiti kutokana na shambulizi hilo na kuwa maisha ya Polisi wenye asili ya Kiafrika ni muhimu kama ilivyo ya polisi weupe.

Rais Obama, ambaye alilaani vikali shambulio hilo aliamuru bendera zote zipeperushwe nusu mlingoti katika majengo yote ya Serikali kwa muda wa siku tano kwa heshima ya maofisa hao.

Ikulu ya Marekani ilisema Rais Obama mara baada ya kukatiza ziara yake jana, siku moja kabla ya ziara yake rasmi kukamilika, ataelekea Dallas kwa mwaliko wa Rawlings.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles