26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mapato ya madini yazidi kupanda

Na JANETH MUSHI -ARUSHA

SERIKALI imesema mapato ya Wizara ya Madini yameongezeka kutoka Sh bilioni 196 mwaka 2016 hadi bilioni 310 mwaka 2018/19.

Kuongezeka kwa mapato hayo, kunatajwa kuchangiwa na marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanywa mwaka juzi na kuanzishwa kwa masoko ya madini.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, alipokuwa akizindua soko la kimataifa la madini jijini hapa.

Alisema mwaka 2018, baada ya marekebisho ya sheria, mapato hayo yalifikia Sh bilioni 265.

“Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kuongeza manufaa ya sekta ya madini kwenye uchumi mkubwa wa nchi, sekta hii imefanyiwa marekebisho mbalimbali ili mchango wa sekta hiyo uzidi kuongezeka.

Alisema awali kabla ya marekebisho hayo mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa ulikuwa mdogo ukilinganishwa na sekta nyingine na kuwa baada ya mabadiliko ya sheria mchango umeanza kukua na kuongezeka.

“Baada ya marekebisho ya sheria mchango wa sekta ya madini umetoka asilimia 3.5 hadi kufikia asilimia 5.07 mwaka 2018 na tunakusudia ikifika mwaka 2025 ufike asilimia 10, na tutafikia kwa sababu hakuna kipindi nasimama nikiwa na furaha nikikutana na wachimbaji kama sasa hivi, wanalipa kodi vizuri.

“Mapato ya juu tuliyowahi kuwa nayo kwenye madini kabla ya marekebisho ya sheria ilikuwa Sh milioni 943, mwaka 2016 hali ilikuwa mbaya zaidi mapato ya juu ya Tanzanite ilikuwa Sh milioni 700. Wachimbaji wadogo peke yao wameshachangia zaidi ya Sh bilioni 2.7, yote hii ni kwa sababu wachimbaji wameitikia wito na kukubali kulipa kodi,” alisema.

Kuhusu mapato ya madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Mirerani mkoani Manyara, alisema baada ya kujengwa kwa ukuta katika eneo hilo, yameongezeka kutoka kilo 147.7 mwaka 2017 hadi kufikia kilo 949.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles