28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mapacha watatu kuwashukuru Bagamoyo

MAPACHA WATATU 1NA MWALI IBRAHIM

BENDI ya muziki wa dansi ya Mapacha Watatu inatarajia kufanya onyesho maalumu kwa ajili ya shukrani kwa mashabiki wao wa Bagamoyo kutokana na kura walizowapigia hadi wakashinda tuzo za kili.

Mmoja wa viongozi wa bendi hiyo, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ alisema, onyesho hilo litafanyika Ijumaa ijayo kwa kutoa nyimbo mbili mpya ambazo ni ‘Mapacha wasasa’ na ‘Wabaya watu’.

“Mashabiki wetu walituwezesha kupata tuzo mbili kwenye mchakato wa tuzo za Kilimanjaro zikiwa ni ‘Mtunzi bora’ na ‘Mwimbaji bora’ zilizokwenda kwa Joseph Mponyezya ‘Jose Mara’.

Alisema, sambamba na utambulisho wa nyimbo hizo, pia watawaburudisha mashabiki hao kwa nyimbo zilizozoeleka ukiwemo ‘Sauti ya marehemu’, ‘Chozi la mwanamume’, ‘Kombe uwanjani’ na ‘Wapenzi walewale’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles