26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mansour apandishwa kizimbani

Aliyekuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki, Mansour Yusuf Himid
Aliyekuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki, Mansour Yusuf Himid

Na Is-haka Omar, Zanzibar

ALIYEKUWA Mwakilishi wa Kiembe Samaki, Mansour Yussuf Himid, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mkoa Vuga, akituhumiwa kutenda makosa matatu likiwemo la kukutwa na silaha pamoja na risasi kinyume cha sheria.

Akimsomewa mashitaka hayo jana  mbele ya Hakimu Khamis Ramadhani,  Mwendesha mashtaka wa Serikali,  Maulid Ali,  alisema Agosti 2, mwaka huu saa 7:18 katika eneo la Chukwani mjini Unguja,  mtuhumiwa huyo alikutwa na bastola ya Beretta yenye namba za F 76172 W.

Alidai kitendo hicho kinakwenda kinyume cha sheria namna 6 (3) na  34 (1) (2) cha sheria  ya silaha na risasi Namba 2 ya mwaka 1991 sura ya 223 ya Sheria ya Jamhuri ya Muungno wa Tanzania.

Kosa la pili ni kupatikana na risasi za moto 295 za bastola jambo ambalo ni kosa kisheria

Pamoja na hali mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa kosa la tatu dhidi ya mtuhumiwa huyo ni kupatikana na  risasi 112 za Short gurn  baadala ya kuwa na risasi 50 kama kwa mujibu wa sheria.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mtuhumiwa Mansour alikana mashtaka hayo.

Kutokana na hali hiyo Mwendesha Mashtaka wa Serikali Maulid Ali, aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo hadi pale ushahidi utakapokamilika.

“Mheshimiwa hakimu tunaiomba mahakama hii tukufu ituongezee muda kwa ajili ya kukamilisha ushahidi wa shauri hili,” alisema.

Kutokana na shauri hilo na upande wa utetezi kuomba mteja wao kupewa dhamana na Hakimu Ramadhani, alikubali ombi hilo na kusema katika makosa mawili anayotuhumiwa nayo kosa moja lina dhamana huku lile la kukutwa na silaha halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

“Mtuhumiwa Mansour makosa mawili yana dhamana isipokuwa moja ndiyo halina dhamana hivyo utarudishwa rumande hadi Agosti 18, mwaka huu huku taratibu zingine za kisheria zikiendelea,” alisema Hakimu Ramadhani.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, Wakili wa Mansour ,  Gasper Nyika, alisema wanakusudia kuwasilisha ombi la dhamana kwa mteja wao Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jeshi la Polisi mjini Unguja lilazimika kuimarisha ulinzi katika viunga vya Mahakaka ya Vuga,  ambapo zaidi ya magari matatu ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), lilipita kila kona ya mahakama.

Askari hao walimsindikiza mtuhumiwa huyo wakati akirudishwa rumande kwa gari zenye namba za usajili PT 1891, PT1456 na 2696 EH .

Mapema jana ilielezwa kuwa, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ataongoza jopo la wanasheria kumtetea Mansour.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Kamati ya Maridhiano, Ismail Jussa, alisema Lissu ataungana na Wakili Fatma Karume ili kumtetea Mansour.

“Wakili msomi na mnadhimu mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni,  Tundu Lissu ataungana na wakili Fatma Karume kumtetea Mansour Himid.

Kutokana na ombi lililowasilishwa na Makama Kuu ya Zanzibar Jeshi la Polisi liliamuliwa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ambapo uamuzi huo ulitolewa na Jaji Abraham Mwampashe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles