27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Manchester United yaongeza dau kwa Maguire

MANCHESTER, England 

KLABU ya Manchester United, ipo  tayari kuvunja benki na kulipa kiasi cha Pauni Milioni 80 (Sh bilioni 223)  ili kunasa saini ya beki wa kimataifa wa England, Harry Maguire kutoka Leicester City .

Ofa hiyo ni pili, kwani Leicester iliipiga chini ya awali iliyo ya pauni milioni 70 (sh bil.195), katika kipindi hiki cha dirisha usajili wa majira ya joto.

United imerudi tena kwa kishindo na kuiboresha ofa yao ili kuishawishi Leicester City kumwachia beki huyo kabla ya dirisha la usajili Ulaya kufungwa Alhamisi ijayo.

Endapo ofa hiyo itakubaliwa, United itakuvunja rekodi ya uhamisho inayoshikiliwa na mahasimu wao, Liverpool, ambao walilipa  Pauni Milioni 75  kumnasa beki, Virgil Van Dijk, ambaye ndiye mlinzi ghali zaidi kwa sasa.

Leicester nayo imepanga kuhakikisha wanapokea zaidi ya ada ya Euro milioni 75 ambayo Liverpool ililipa Southampton kwa Dijk mwaka jana.

United wana shauku ya kupata saini ya Maguire haraka iwezekanavyo, lakini wataelekeza mawazo yao mahali pengine ikiwa hawawezi kukamilisha mpango huo.

Hata hivyo, Maguire  amemwambia kocha wa Leicester, Brendan Rodgers na maofisa wa klabu hiyo kwamba anataka kujiunga na United.

United inataka kukamilisha uhamisho huo haraka baada ya Eric Bailly kukosekana kwa miezi mitano kutokana na kuuguza majeraha ya goti, hivyo wanahitaji beki wa kati wa kuziba pengo lake.

Hadi sasa, United imefanikiwa kunasa wachezaji wawili ambao ni beki wa kulia, Aaron Wan-Bissaka kutoka Crystal Palace  na winga, Daniel James aliyetokea Swansea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles