26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane kutomchezesha tena Bale

Munich, Ujerumani

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Gareth Bale, atamaliza msimu ujao bila kucheza kutokana na kocha timu hiyo, Zinedine Zidane kuweka wazi kuwa hatamchezesha tena nyota huyo.

Zidane ameendelea kuonyesha kuwa nyota huyo si chaguo lake baada ya kusema hakikuwa kitendo cha dharau kwa mchezaji kuonekana akicheza gofu wakati kikosi kikipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Spurs katika mchezo wa Kombe la Audi Jumanne.

Bale alikaribia kutimkia China ambapo angekuwa akilipwa mshahara wa Euro milioni moja (Sh. bilioni 2) kwa wiki, lakini mpango huo ulikufa baada ya dirisha la usajili la nchi hiyo kufungwa jana, huku mwenyewe akionyesha wazi kuwa hayupo tayari kucheza chini ya Zidane. 

Zidane naye amebainisha wazi kuwa hatamtumia Bale katika kipindi chote atakachokuwa kocha wa timu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Wales, amebakiza mkataba wa miaka mitatu wa kuendelea kubaki katika viunga vya Santiago Bernabeu, akilipwa mshahara wa Euro 650,000 kwa wiki, huku akikataa kata kata kutolewa kwa mkopo.

Bale anaonekana kukwama kuondoka katika klabu hiyo kipindi hiki cha kiangazi, huku akiwa nje ya kikosi kutokana na kutosafiri na timu kwenda Munich kwa ajili Kombe la Audi.

Licha ya Zidane kusema kuwa Bale alikuwa mgonjwa, mchezaji huyo aliwaambia Madrid  kwamba, kiakili, hakuwa katika hali ya kucheza kutokana na Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez kukwamisha uhamisho wake wa kujiunga na Jiangsu Suning.

Hata hivyo, alionekana akijipumzisha mbali na wachezaji wenzake baada ya timu hiyo kupoteza mbele ya timu yake ya zamani, kitendo ambacho kilitafsiriwa na mashabiki wa timu hiyo pamoja na vyombo vya habari nchini Hispania kama utovu wa nidhamu.

Akizungumza baada ya kuiongoza Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 5- 1 dhidi ya Fenerbahce katika mchezo wa tatu uliochezwa kwenye Uwanja wa Allianz, Zidane, alisema: “Sijui chochote kuhusu hilo, sijaona picha kwa hivyo siwezi kusema mengi kuhusu hilo.

“Nadhani anafanya kazi vizuri na tutaona tutakaporudi. Sitamwambia aache au kwamba hairuhusiwi kucheza (gofu), yeye ni mtu mzima, anaweza kufanya kile anachotaka.

“Ni maisha yake ya kibinafsi, sitamuhukumu kwa chochote,” alisema Zidane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles