MIAMI, MAREKANI
KLABU ya Manchester City imejaa hofu juu ya mshambuliaji wake mpya Riyad Mahrez, kuwa anaweza kuukosa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa Jumapili ijayo dhidi ya wapinzani wao Chelsea.
Mchezo huo ni dalili ya kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu nchini England, lakini Mahrez anaweza kuukosa kutokana na kupata majeruhi jana alfajili kwenye mchezo wao dhidi ya Bayern Munich.
Mchezaji huyo ambaye amejiunga na Manchester City katika kipindi hiki cha majira ya joto akitokea Leicester City kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 60, aliisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, lakini alipata tatizo la enka.
“Sijui atakuwa nje kwa muda gani, najua amepata tatizo la enka, lakini tutaona labda hakupata tatizo kubwa sana, kitu ambacho kinanipa wakati mgumu ni kuona mchezaji anaumia, huku wachezaji wengine wakiwa bado wapo kwenye mapumziko baada ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.
“Siwezi kuwalaumu wachezaji ambao bado hawajawasili, lakini ninafurahia kile walichokifanya kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Mahrez anaweza kuukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea, lakini ninaamini tuna kikosi kipana kuweza kuziba nafasi hiyo,” alisema Guardiola.
Hata hivyo kocha huyo alieleza sababu ya kumuacha benchi mshambuliaji wake wa pembeni Leroy Sane baada ya kucheza katika mchezo wa kwanza dhidi ya Liverpool.
“Sane bado hayupo sawa kiakili, hivyo anatakiwa kufanya mazoezi taratibu ili kuweza kurudi katika ubora wake, lakini wala hana majeruhi yoyote kama watu wanavyodhani,” aliongeza