28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mamia wajitokeza kumzika Ebby Sykes

sykesNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
SAFARI ya mwisho ya aliyekuwa mkongwe wa muziki wa Ragger nchini ambaye pia ni baba mzazi wa msanii, Dully Sykes, Ebby Sykes (62), imehitimishwa jana kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Mkongwe huyo alifikwa na umauti juzi mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa vidonda miguuni vilivyodaiwa kueneza sumu mwilini mwake kutokana na matumizi ya uvutaji wa sigara.
Wasanii mbalimbali wameonyesha kusikitishwa na kifo hicho na kujitokeza kwa wingi kufanikisha mazishi ya msanii huyo.
“Baba alikuwa rafiki yangu, kifo chake ni pigo kwetu wote kwani kwa kiasi kikubwa amekuwa akitusaidia na kutupa mwangaza wa kuendesha muziki wetu,” alisema Dully Sykes.
Mbali na msanii huyo, wasanii wengine waliweza kutoa salamu na pole kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles