Nisha kuwapa elimu ya maisha mashabiki

0
1284

nishaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
MWIGIZAJI wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’, amesema anatarajia kuachia kazi yake mpya aliyoipa jina la ‘Shida’, ambayo itatoa mafunzo kwa mashabiki kukabiliana na hali yoyote ya maisha.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Nisha alisema filamu hiyo inatarajia kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ameweza kumshirikisha nguli mwingine, Gabo.
“Mashabiki wakae tayari kwa ujio wangu mpya naamini watajifunza vitu vingi vinavyohusu maisha yetu ya Kitanzania kupitia filamu hii ya Shida,” alisema Nisha.
Alisema mashabiki wategemee mambo mengi mazuri zaidi kutoka kwake, kwani mara nyingi amekuwa akifanya kazi kwa mpangilio ili kuhakikisha anatoa vitu vyenye ubora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here