23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mamia wajitokeza kumuaga Hans Poppe Dar

Na Salome Bruno, Tudarco

WANACHAMA wa Simba na wadau mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ludigija, wamejitokeza kuaga mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe kwenye viwanja Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hans Poppe, aliyefariki Septemba 11 katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Saaam alipokuwa akipatiwa matibabu anatarajiwa kuzikwa Jumatano nyumbani kwamo Iringa.

Akizungumza wakati wa kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaa, Ludigija amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma salamu za pole kwa familia ya Hans Poppe, nakuwataka kushikamana.

“Wanafamilia hiki ndio kipindi muhimu ambacho mnatakiwa kushikamana kuliko kipindi kingine chochote na muamini kuwa sio nyie pekee mliofiwa bali ni wote na ndio maana tumekusanyika hapa kufarijiana.”amesema Ludigija.

Kwa upande wake Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodiga Tenda ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT), amesema Hans Poppe alikuwa anapenda mchezo unaopendwa na watu wengi.

“Tunapomuaga Hans Poppe ni kama tunasherekea miaka yake 65, mchezo aliokuwa anaupenda unakutanisha watu wengi,” amesema.

Naye Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori
Amesema kuwa marehemu akiwa na umri wa miaka 28 tayari ni kapteni wa Jaeshi na alitaka kupindua, umri ambao wengine wanakuwa bado wanaishi na wazazi nyumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles