24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge ashauri kuwepo sheria ya chakula

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia kundi la asasi za kiraia (NGO’s),Neema Lugangira,amesema Tanzania inahitaji Sheria ya Usalama wa Chakula na suala hilo kusimamiwa chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii Wazee Jinsia na Watoto.

Mbunge huyo ameyasema hayo mwishoni mwa wiki akichangia Azimio la kuridhia itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya viwango vya afya ya mimea,afya ya wanyama na usalama wa chakula.

Amesema ni vema suala la usalama wa chakula kuwa chini ya wizara hiyo, ili kukidhi matakwa ya itifaki hiyo.

“Mchango wangu utajikita eneo zima la usalama wa chakula,kwanza kabisa ningependa kuishauri serikali kwenye eneo zima la usalama wa chakula kuratibiwa chini ya Wizara ya Afya,  ni kuona namna gani ambavyo utalinda walaji wasipate changamoto zozote zinazotokana na chakula.

“Naipongeza wizara ya kilimo kwa sababu wameimarisha usimamizi   kwenye afya ya mimea chini ya TPRI,kwani moja ya matakwa ya itifaki hii duniani ni lazima nchi iwe na sheria ya usalama wa chakula, Tanzania bado hatuna,” amesema Mbunge huyo.

Neema amesema ndani ya nchi za EAC ni Kenya peke yake ambayo tayari wana sheria ya usalama wa chakula, hivyo Tanzania kuendelea kukosa sheria hiyo haitaweza kunufaika.

 “Naomba nishauri serikali baada ya azimio hili kuridhiwa  usimamizi wa masuala ya afya ya mazao ya kilimo yatakuwa chini ya Wizara ya Kilimo,”ameongeza.

Amesema ni muhimu wakulima na wananchi kwa ujumla kupewa elimu ya itifaki hiyo ili waweza kukidhi vigezo vyake na kunufaika nayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles