23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBOSASA AJA NA MIKAKATI KUKABILI UTEKAJI DAR

PATRICIA KIMELEMETA

Na MAMII MSHANA (TURDAco)

-DAR ES SALAAM

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amekuja na mikakati kadhaa ya kuweza kukabiliana na uhalifu jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Mambosasa alisema suala la uwepo wa vitendo vya utekaji vinavyofanywa na watu wasiojulikana halitafumbiwa macho tena, hivyo kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe haraka.

Alisema kwa sasa atalifuatiliwa kwa kina suala hilo ili aweze kujua vyanzo vya baadhi ya watu wakiwamo wasanii kutekwa ili aweze kuwachukulia hatua wahusika.

Alisema katika kipindi chake cha uongozi akiwa mkoani humo, atashirikiana na watendaji mbalimbali wakiwamo wanasiasa, viongozi wa dini, polisi jamii na wananchi wa kawaida ili kuhakikisha wanaendesha msako wa kuwakamata wahalifu hao.

Alisema anatambua kuwa kuna kamati za ulinzi na usalama kuanzia ngazi ya mkoa hadi kata, hivyo basi atashirikiana nao ili kuhakikisha anapata taarifa za wahalifu hao pamoja na kuwachukulia hatua.

Alisema lakini pia kuna makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi ambayo na yenyewe anapaswa kuwa nayo karibu ili waweze kuhakikisha ulinzi unaimarika katika mkoa huo.

Akizungumzia kuhusu baadhi ya askari polisi wanaotumia nafasi zao kwa ajili ya kunyanyasa wananchi, alisema wananchi watakaokumbwa na kadhia hiyo watoe taarifa ili watakaobainika wachukuliwe hatua.

Alisema anatambua haki za binadamu na utawala bora, hivyo basi hawezi kuona baadhi ya askari wanatumia nafasi zao kwa ajili ya kuwanyanyasa wananchi na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua.

“Tuna taarifa za kuwepo kwa baadhi ya askari ambao wanatumia madaraka yao vibaya kwa ajili ya kunyanyasa wananchi, huku wakitambua kuwa, kitendo hicho ni kinyume na kifungu namba 5 cha sheria ya makosa ya jinai, siwezi kuvumilia suala hilo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles