23.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mambo 5 Usiyoyajua kuhusu MABESTE,LISA

mabesteNA CHRISTOPHER MSEKENA

MARA nyingi tunapenda kuwafahamu watu maarufu nje ya maisha yao ya sanaa, licha ya kutamani kuwafahamu
imekuwa ngumu kutokana na mastaa hao kutoonekana mara kwa mara kitaa kwa lengo la kuongeza mvuto
kwenye jamii.
Swaggaz wiki limetua maskani mwa nyota wa muziki wa rap, Venance  maarufu kama Mabeste na ametuambia
mambo yake kumi ambayo hujawahi kuyasikia popote, kama uliyasikia basi hapa anakueleza vizuri.

ALIVYOJUANA NA PANCHO

Mabeste anasema yeye na Pancho walikuwa marafiki wa muda mrefu toka kipindi cha dhadabu Records studio inayomilikiwa na Dully Sykes.
Pancho ndiye aliyemuita Mabeste aje Bongo wafanye kazi kwa sababu kipindi hicho Mabeste alikuwa anaishi
Kenya.
“Pacho ndiyo alinitoa Kenya, nilikuwa na mzuka wa kusikika lakini nilipofika mambo yalikuwa tofauti, nilirekodi nyimbo nyingi lakini B Hits wakasema kiwango changu bado ni kidogo, mpaka wimbo wa Baadae Sana unatoka kiukweli nilikuwa nimekata tamaa na muziki,” anasema.

DULLY NDIYO ‘GOD FATHER’ WAKE

Mshkaji anasema kipindi chote alipokuwa anahangaika kuhusu muziki mkongwe Dully Sykes ndiyo alikuwa msaada kwake, kuanzia kuvaa, kula na kulala aliishi nyumbani kwa Dully kwa muda mrefu, hivyo anamtazama Dully kama ‘God Father’ wake kwenye muziki.

LISSA NI SEHEMU YAKE.

Mkali huyu anasema Mungu ndiyo anajua kama Lisa Karl Fickenscher atakuwa mke wake au laa, lakini mpaka hapo walipofika Lissa ni sehemu yake kwa kuwa ni mzazi mwenzake hivyo hata kama wataachana bado mrembo huyo
atakuwa ni sehemu ya maisha yake.

HAJAWAHI KUYUMBA KIMAISHA

Kuna stori zilikuwa zimesambaa kuwa Mabeste alipoteza uelekeo mara baada ya kuondoka B Hits, mwenyewe anasema kimuziki alishuka lakini hajawahi kuyumba kimaisha.
“Niliondoka B Hits nikiwa nimepanga chumba kimoja hata Tv sina, lakini nilipoanza kufanya kazi zangu mwenyewe
nikahama Mbagala nikahamia Kinondoni nikapanga upande mzima wa nyumba, nikanunua gari na maisha
yakaendelea kama kawaida, kwa hiyo kimuziki nilishuka lakini sikuyumba kimaisha,” anasema

ANAMTENGENEZA KENDRICK KUWA STAA

Mabeste anasema kuna kitu zaidi ya kipaji anakiona kwa mwanae anayeitwa Kendrick, ndiyo maana amekuwa mstari wa mbele kumkutanisha na watu mbalimbal maarufu pamoja na kumuingiza kwenye mashindano ya watoto.
“Nikiwa kama baba lazima nitambue mwanangu anakipaji gani, mzazi anaweza akajenga au akabomoa uwezo wa mtoto wake kufanya jambo kubwa kwenye jamii, Kendrick ninamkuza kutokana na kile kitu anachokipenda”
anasema.

Hayo ndiyo mambo ambayo Swaggaz limekuandalia leo hii hapa kwenye kwenye Bongo Fleva, tumemleta Mabeste leo kwa sababu ndani ya mwaka huu yeye na mpenzi wake Lisa Karl Fickenscher walipitia magumu mengi lakini bado wameendelea kuopendana,  Swaggaz linawatakia maisha mema mwaka ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles