21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kinguti System’ nyota inayongaa nchini Thailand

Ramadhani KingutiNA VALERY KIYUNGU,

KARIBU msomaji wa safu hii ya Tujikumbushe inayokujia kila siku za Jumamosi, hapa tunapata nafasi ya kuwachambua wasanii mbalimbali waliofanya vizuri miaka ya nyuma kwa lengio la kizazi kipya kijiifunze mengi kutoka kwao.

Wiki hii nipo na mwanamuziki, mtunzi na mpigaji ala za muziki, Ramadhani Kinguti maarufu kama Kinguti System ambaye hivi sasa anafanya vizuri katika tasnia hiyo ya muziki nchini Thailand.

Kwa mujibu wa swahiba wake wa karibu ambaye ni mwanamuziki mwandamizi wa bendi ya Sikinde, Abdallah Hemba amedhibitisha ujio wa nyota huyo wa dansi katika maadhimisho ya miaka 37 toka bendio hiyo kongwe ianzishwe.

Kinguti System ni mzaliwa wa Ujiji huko mkoani Kigoma ambapo safari yake ya muziki ilianza mwaka 1977 na bendi yake ya kwanza kuitumikia ilikuwa inaitwa Super Kibisa ambayo ilikuwa maarufu sana kipindi hicho mkoani Kigoma.

Binamu yake anayeitwa Mlolwa Mussa Mahango ndiyo aikuwa akiimiliki bendi hiyo hivyo undugu huo baina yao ulimuwezesha Kinguti System kuingia Super Kibisa bila tabu yoyote na hapo ndipo kipaji chake kilianza kung’aa.

Wakali kama Golo Saidi, Haruna Mahepe, na Maulidi ndiyo walikuwa washika dau wakubwa kwenye bendi hiyo na walimpa ushirikiano mkubwa uliochangia kuboresha kipaji chake.

Kama niliposema hapo awali, Kinguti siyo mwanamuziki tu bali ni mtunzi wa mashahiri akiwa Super Kibisa alitunga nyimbo kali kama vile Mapenzi Tabu, Zaina pamoja na Kazi ni Uhai.

Shaabani Dede alipohama Dodoma International na kuhamia JUWATA Jazz ambayo hivi sasa inajulikana kama Msondo mwaka 1979, ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Kinguti System kuhamia kwenye bendi hiyo yenye makazi yake Dodoma.

Akiwa kwenye bendi hiyo alikutana na nyota Kassim Rashid ‘Kizunga’ na hiyo ilikuwa kabla hajahamia Orchestra Makassy ambako pia mastaa kama Remmy Ongara, Masiya Adi, Andy Swebe, Keppy Kiombile, John Kitime, Issa Nundu, Kyanga Songa, Choyo Godjero  na Mzee Aimala Mbutu walikuwa wakifanya yao.

Alidumu kwa mika kadhaa na hapo mwaka 1986 alijiunga na bendi ya Afrisongoma iliyokuwa ya Lovy Longomba na huko nako alijizolea umaarufu kwa kutunga ngoma kali kama Pesa Maua, Amana Mpenzi na Estah Usitochonganishe.

Baada ya hapo alijiunga na DDC Mlimani Park ambako licha ya kukaa na bendi hiyo kwa kipindi kifupi, alivuma utunzi wa wimbo wa Visa Vya Mwenye Nyumba wimbo ulioibwa na wakali Hassan Bitchuka, Francis Lubua, Hussein Jumbe na Bennovills Anthony.

Mwaka 1989 Kinguti System alitua ndabni ya bendi ya Bicco Stars ambapo miaka kumi baadae alijiunga na Kilimanjaro Connection bendi ambayo ilikuwa ni ya mwisho kuitumikia na baada ya hapo alijichanga na kuanzisha bendi ayke inayoitwa The Jambo Surviovors bendi ambayo inafanya poa mpaka leo hii hiko nchini Thailand.

    *Maoni na ushauri leta hapa 0714 288 656*

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles