24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAMA WEMA ATOA MSIMAMO HATIMA YAKE CHADEMA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


MAMA mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Miriam Sepetu amekanusha taarifa zilizombazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na mwanawe wana mpango wa kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Februari 25 mwaka huu Wema na mama yake Miriam walijivua uanachama wa CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kwenda kupigania demokrasia ya kweli.

Juzi katika mitandao ya kijamii zilianza kusambaa taarifa kuwa Wema na mama yake wana mpango wa kurudi CCM kwa madai kuwa wameahidiwa kutobomolewa nyumba yao na Wema kufutiwa kesi inayomkabili mahakamani ya matumizi ya dawa za kulevya.

Akiandika katika mitandao ya kijamii jana, mama Wema alieleza yeye na mwanaye wataendelea kuwa wanachama wa Chadema na mwanaye.

“Mimi ninachoona CCM wana akili ya kutaka kuvuruga Chadema. Na tuwe makini kwa maneno ya kutuvuruga kwa kipindi hiki tujenge chama.

“Kuna watu ambao si waelewa kabisa na CCM wanajua nguvu ya Wema na yangu zilivyo, waje  wabomoe nyumba. ‘Notes’ wametoa lini ya kubomolewa hii nyumba? Basi kifo cha wengi ni harusi.

“Mimi nitakuwa Chadema pamoja na mwanangu na mimi ndiye msemaji mkuu. Wao waje wabomoe tu nipo tayari. Kwanza hawanibomoi mimi. Wana bomoa nyumba ya marehemu Sepetu,”alisema mama Wema.

Wakati wakijiunga na Chadema, walisema wamejiunga na chama kilichoisumbua CCM wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Naye Wema alisema alijiunga Chadema bila kulipwa chochote na iwapo ikibainika kinyume kaburi la baba yake Zanzibar lipasuke katikati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles