24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NAIBU WAZIRI ANUSURIKA SHAMBULIO LA GESI

Na PETER FABIAN-MWANZA


NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula jana alinusurika kudhurika katika shambulio la gesi ya kuwasha.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA kutoka ukumbi wa mikutano wa Rocky City Mall, ulikokuwa ukifanyika uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM, (UVCCM) zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea jana, majira ya saa 6 mchana.

Baadhi ya washuhuda walilieleza gazeti hili kuwa wakati wajumbe wa mkutano wakiwa ndani ya ukumbi wakiimba nyimbo za chama kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongela hali ya hewa ilibadilika.

Walisema wajumbe walianza kukohoa na kupiga chafya huku wengine wakiwashwa mwilini hali iliyosababisha taharuki ndani ya ukumbi.

Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo aliyezungumza kwa sharti la jina lake kutotojwa gazetini alisema gesi hiyo ilipulizwa na mtu asiyefahamika ambapo wajumbe walianza kukimbuilia nje kwa ajili ya kujiokoa huku Naibu Waziri Mabula akisaidiwa kutoka nje alikopatiwa huduma ya kwanza.

Alisema Naibu Waziri Mabula alisaidiwa kutoka nje na walinzi wa chama (Green Guard) ambao baada ya kuhahakisha usalama wake walianza kuwasaidia wajumbe wengine waliokuwa na hali mbaya.

“Hali ilikuwa tete maana la tukio la dakika 30 lakini lilikuwa hatari kwa sababu wajumbe baada ya kuzidiwa na muwasho, baadhi yao walianza kuanguka na kukanyangwa na wenzao waliokuwa wakikimbilia nje kujiokoa.

“Wajumbe wengi walifanikiwa kutoka nje walikopatiwa huduma ya kwanza pamoja kutafutiwa maziwa na maji ili kuondoa mathara ya gesi mwilimi,” alisema.

Habari zinasema Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala alifanya kikao cha dharura na Mkuu wa Mkoa, Mongela na kukubaliana mkutano huo uhamishiwe uwanja wa CCM Kirumba.

“Baadaye polisi walikuja na kuanza upekuzi kwa baadhi ya wajumbe waliokuwa na mabegi na mikoba, wakamkamata mjumbe mmoja waliyetaka kuondoka naye kwa mahojiano.

“Kijana aliyekamatwa alikuwa na chupa ya marashi ambayo waliifananisha na gesi ya kuwasha, hata hivyo vurugu zilianza ambapo baadhi ya wajumbe na wakishinikiza mwenzao aachiwe.

“Mkuu wa Mkoa ilibidi aingilie kati kuwatuliza vijana na kuamuru polisi wamuachie mjumbe waliyekuwa wamemkamata kisha mkutano ukaendelea,” alisema mjumbe mwingine ambaye pia hakutaka jina lake litajwe.

Alipoulizwa Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Mwangwala kuhusu tukio alisema hali ya utulivu ilirejea baada ya muda mfupi wa taharuki.

“Nipo huku kuna kelele kidogo hatuwezi kusikilizana ila hali ni tulivu na tunaendelea na mkutano baada ya kuhamia CCM Kirumba,” alisema Mwangwala.

Naibu Waziri, Mabula alipoulizwa yeye alisema yupo vizuri kwa sababu aliwahi kutoka ndani ya ukumbi kisha akawasiliana na Mkuu wa Mkoa, Mongela ambaye aliwasiliana na polisi.

“Sijajua kama kuna watu wameumia zaidi ila nilichoona ni wengi walikuwa wakikohoa na kutoa machozi kutokana na kuwashwa na gesi hiyo, sikuwa na madhara kwa sababu niliwahi kutoka ndani ya ukumbi.

“Nimesaidiwa sana na mbinu za JKT hivyo haikunipa taabu kujiokoa lakini vijana pia walikuwa tayari kunisaidia,” alisema Naibu Waziri Mabula

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles