24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mama wa Dogo Aslay azikwa Dar

ASLAYNA MELCKZEDECK SIMON

MSANII kiongozi wa kundi la Yamoto Band, Aslay Isihack ‘Dogo Aslay’ jana alijumuika na wadau mbalimbali wa sanaa kumzika mama yake mzazi, Moza Mohammed aliyefariki juzi hospitali ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Mama wa msanii huyo alifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Temeke, alipokuwa amelazwa.

Wadau mbali mbali wa muziki walimpa pole msanii huyo kutokana na kuondokewa na mama yake kipenzi ambaye alimtimizia kumjengea nyumba kutokana na kipato chake cha muziki.

Katika hatua nyingine video ya wimbo wao mpya ya ‘Cheza Kimadoido’ ya kundi lao inaelezwa kugharimu zaidi milioni 30 fedha za Tanzania.

Akizungumzia kuhusu video hiyo, mkurugenzi wa kundi hilo lenye maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam, Saidi Fella, amesema gharama hizo zimekuwa kubwa kwa kuwa walitaka iwe na utofauiti na video za wasanii wengine katika ubora ili iweze kupenya katika soko la kimataifa.

“Kampuni ya Godfather ya Afrika Kusini ndiyo imesimamia kazi hiyo na tunaamini tutavuka mipaka na kufanya vema kimataifa kama tunavyofanya vizuri hapa nchini,” alieleza Fella ambaye naye anagombea udiwani Kata ya Kilungule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles