27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Malinzi ashangaa kushtakiwa kwa kuikopesha TFF

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amedai wanaolikopesha shirikisho hilo ni wengi, lakini anashangaa yeye kushtakiwa wakati ni jambo la kawaida tangu miaka ya 60.

Amesema kukopa kwa Klabu ya Simba na Yanga pia ni kawaida. Akatolewa mfano Klabu ya Simba ilikopa Sh bilioni Sita kwa Mohammed Dewji ambaye aliwasamehe wakati wa uzinduzi wa uwanja wao wa Bunju.

Malinzi anayekabiliwa na mashtaka ya kughushi na kutakatisha fedha amedai kuwa, aliikopesha TFF kwa nyakati tofauti bila kudai riba na kwamba alilipwa deni kwa mafungu kulingana na upatikanaji wa fedha.

Utetezi huo aliendelea kuutoa jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.

Akiongozwa na Wakili Richard Rweyongeza, Malinzi alidai taasisi zote za soka, Klabu ya Simba na Yanga, vyama vya soka vya wilaya na mikoa kukopa, hivyo ni utaratibu wa kawaida.

Alidai hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa Uwanja wa Simba Bunju, Mohammed Dewji alisamehe deni la Sh bilioni sita alizoikopesha Simba kwa matumizi mbalimbali, ikiwemo usajili.

Alidai utaratibu huo uko miaka mingi lakini yeye ni wa kwanza kushtakiwa kwa sababi hiyo.

Malinzi aliwataja wengine wanaokopesha kuwa ni Ahmed Mgoy, ambaye aliikopesha TFF Sh milioni 55 na Mkurugenzi wa Fedha,  Daniel Msangi alithibitisha hilo mahakamani wakati akitoa ushahidi.

Anadai akiwa kama kiongozi na familia ya TFF,  aliwajibika kutoa fedha zake ikiwamo kuitumia Dola za Marekani 7,000,  timu ya Taifa ‘Taifa Staa’ ilipokwama nchini Zimbabwe.

Alidai kuwa alikamatwa Juni 27, akiwa kwenye usaili kama mgombea urais na kukaa mahabusu ya polisi mpaka Juni 29,2017 aliposomewa mashtaka yanayomkabili kwa mara ya kwanza na kwamba Julai Mosi, mwaka huo alitenguliwa wadhifa wake kama rais.

Alidai kuwa Makamu wake,  Wales Karia aliitisha mkutano wa Kamati ya Utendaji Julai Mosi,2017, walimuengua nafasi yake, walikata jina lake kama mgombea urais,waliivunja kamati ya uchaguzi na kumpitisha Karia kama mgombea pamoja na kuteua kamati mpya ya uchaguzi.

Alidai kuwa kitendo cha kumuengua na kuvunja kamati hiyo ni kinyume cha kanuni na katiba ya TFF.

Malinzi ambaye aliomba kibali cha mahakama kunywa fundo kadhaa za soda aina ya cocacola na kukubaliwa, alidai kuwa mwenye mamlaka ya kuitisha mkutano wa kamati ya utendaji ni, Rais na si vinginevyo

“Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Rais ataenguliwa endapo tu atajizulu, kukosa vikao vinne vya Kamati ya Utendaji, kutokushiriki kazi za TFF na kufungwa au kuhukumiwa kulipwa faini.

Lakini mimi niko mahabusu, nimeenguliwa kinyume cha katiba yetu,”alidai Malinzi wakati akiendelea kupigania tuhuma zinazomkabili.

Akizungumzia jinsi alivyolipwa madeni na kupewa risiti, shahidi alidai kuwa,  Mhasibu Mkuu Daniel Msangi alijiridhisha matumizi yake ndipo alilipwa deni lake na shirikisho hilo.

Alidai wakati anapewa fedha alikuwa akipewa risiti kwa majina yake na kwamba aliendelea kutoa fedha hadi alipokamatwa mwaka 2017.

Alidai kuwa risiti hizo zilisainiwa na Hellen Adam ambaye alikuwa shahidi wa kumi wa upande wa mashitaka na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Msangi ambaye alikuwa shahidi wa sita.

 Risiti nyingine haikuwa na saini lakini kwenye taarifa ya benki ilinyesha imeingizwa kama mkopo.

Alidai risiti zote zinatunzwa na idara ya uhasibu ya TFF na kwamba,  alikuwa akilipwa kwa mafungu kutokana na hali ya shirikisho hilo kuwa mbaya kiuchumi.

Aliendelea kudai kuwa,  idara ya fedha ilikuwa ikikaa na kuangalia namna ya kumlipa kutokana na kile wanachokipata.

Kesi ya msingi  namba 213/ 2017, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 20,  yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles