27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAKOSA YANAYOFANYWA NA WANAFUNZI WA KIMATAIFA

Na Joseph Lino


KUWA mwanafunzi mpya katika chuo kikuu nje ya nchi ni jambo moja la kusisimua katika maisha ya mwanafunzi.

Wanafunzi wengi hujisahau au kujaa na hofu hasa wakiwa katika mazingira ya ugenini.

Kuanzia anapokubaliwa kujiunga chuo hatua inayofuata ni kuelewa mazingira halisi ya maisha ya chuo.

Utagundua huwa mitindo ya maisha tofauti katika chuo na nchi hiyo na hii itakusaidia kujifunza kuhusu maisha yako mwenyewe.

Lakini wanafunzi wengi hufanya makosa mbalimbali ambayo husababisha mtu kushindwa kutimiza lengo lake pamoja na kufeli masomo.

Kama mwanafunzi upo makini katika masomo ukizingatia umesafiri masafa ya mbali kuna vitu kadhaa vya kuzingatia ambavyo vinakupa picha halisi ya maisha katika nchi hiyo ya kigeni.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu ambayo wazazi, wakala wa vyuo vya nje au walimu wanashindwa kuelezea kabla haujajiunga chuo.

 

Jaribu kutumia vizuri kila senti unayotumia juu ya elimu yako

Wanafunzi wengi wa kimataifa wanadahiliwa  kupitia udhamini, fedha ya msaada au ‘scholarship’, hivyo inaeleweka kwamba unatakiwa ujitahidi kuweka kila senti unayopata.

Kuwa makini na matumizi ya pesa yako kila mara na kukwepa gharama zisizo za msingi. Inaweza kukuletea msongamano wa mawazo pia.

 

Kutozungumza au kuuliza lolote

Hata hivyo, ingawa baadhi ya wanafunzi wanajitahidi kusoma,  wakati huo huo wanakuwa na hofu ya kuuliza kitu ambacho anataka kutoka kwa watu wa karibu au profesa.

Mara nyingi, tamanduni za ulikotoka zinaweza kukufanya hivyo kwa kujaa na hofu ya kuuliza mahitaji yako.

Hata hivyo, chuo ni sehemu ambayo watu hawahoji vitu ambavyo una faida navyo, lakini wapo wa kusaidia kama utasema kuwa ni mwanafunzi wa kimataifa na mara nyingi unapokelewa vizuri.

Kama ukionekana unasoma kwa juhudi unaweza kupata msaada kwa watu kama utawauliza.

 

Kujihusisha katika uhusiano wa kimapenzi

Kujiingiza katika uhusiano wakati ndio kwanza unaanza chuo si uamuzi sahihi wa kufanya, ni jambo ambalo linaweza kuchukua muda wako ambao ungekuwa unajenga mtandao wa marafiki na watu wengine na inakupunguzia wigo wa maisha yako katika jamii.

Hata hivyo, chuo si sekondari ambako unaweza kuwa darasani na mpenzi wako, muda ambao mtakuwa pamoja ni mchache kwenye chuo kwa sababu kila mmoja ana malengo na vipaumbele tofauti.

Mtu ambaye anahusika na maendeleo ya taaluma yako katika maisha yako ni wewe kwa hiyo unahitaji kufanya uamuzi sahihi.

Kuweka matarajio yako chini ya kiwango

Mazingira ya chuo ni tofauti na sekondari, kama unadhani kuwa uwezo wako sekondari ulikuwa wa kawaida, itakuwa vigumu kufanya vizuri chuo, lakini kama utajiongeza kwa kufanya juhudi za ziada lazima utafanikiwa.

Lakini unatakiwa kuongeza juhudi uwezavyo kwenye masomo na katika mazingira ya kawaida kwa kupata uelewa wakutosha na ujuzi kuanzia mwanzo, kitu cha muhimu ni kwamba watu kama hawa hufanikiwa kuliko wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles