30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAKOSA 285 YAWATIA HATIANI VIGOGO CWT

Vigogo watatu wa Chama cha Walimu cha kukopa na kuweka (Saccos),  Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, kwa ubadhirifu wa fedha na kujipatia zaidi ya Sh milioni 50 za chama hicho kwa kughushi nyaraka mbalimbali.

Vigogo hao waliopandishwa kizimbani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani humo ni  aliyekuwa Ofisa Mikopo wa chama hicho, Gerald Msacky, Mhasibu wa chama hicho, Peter Ndelianarua na Karani wa Fedha, Rehema Lucas. 

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa 281 ya ubadhirifu na ufujaji wa fedha wa chama hicho cha kuweka na kukopa, huku pia wakishitakiwa na makosa 4 ya kughushi nyaraka. 

Mshitakiwa wa pili ambaye alikuwa ni Ofisa Mikopo wa chama hicho anatuhumiwa kutenda makosa 285 huku mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Mhasibu na mtuhumiwa wa tatu, aliyekuwa Karani wao kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makosa 142 kila mmoja. 

Washtakiwa hao kwa nyakati tofauti wanadaiwa kufuja fedha za chama hicho zaidi ya Sh milioni 50. Upelelezi wa kesi hiyo unaendelea ambapo imepangwa tena kutajwa Desemba 28, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles