26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

MAKINDA AWAKEMEA WANAUME WALEVI

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

SPIKA Mstaafu, Anne Makinda, amewataka wanaume wanaotumia fedha zao kunywea pombe huku familia zikiwa hazina usalama wa matibabu ya uhakika, waache tabia hiyo.

Makinda, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), badala yake aliwataka wanaume hao kuacha au kupunguza matumizi ya pombe na waelekeze fedha zao kufungua bima za afya kwa familia zao.

Makinda alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi, alipokuwa katika Parokia ya Mtakatifu Theresia, Jimbo Kuu la Arusha, wakati wa ibada ya shukrani ya Padri Damian Ndege, aliyepata upadrisho Julai 13, mwaka huu.

Akizungumza kwenye ibada hiyo, Makinda alisema moja ya mambo anayotamani katika uongozi wake wa Bodi ya NHIF, ni kuona ameacha asilimia 80 ya Watanzania wakiwa wanatibiwa kwa mfumo wa bima ya afya.

“Niwasihi akina baba walevi wanaotumia hovyo fedha kunywa pombe huku familia zikiwa hazina uhakika wa matibabu, wapunguze pombe na ikibidi waache kabisa kunywa pombe.

“Badala yake, nawaomba mtumie fedha hizo kuweka uhakika wa matibabu kwa walio ndani ya familia zenu kwa kuwafungulia bima ya afya.

“Hili si la kupuuza, kwani hata nchi zilizoendelea, wanatibiwa kwa bima na NHIF inapokea watu kutoka makundi yote.

“Moja ya vitu vya msingi vya kufanyia fedha hizo mnazopata ni kuwekeza kwenye afya ili ndugu au mwanafamilia anapougua, usipate homa ya kutafuta fedha iliyojificha, badala yake utumie kadi ya bima kupata huduma,” alisema Makinda.

Pamoja na hayo, Makinda alitumia fursa hiyo pia kuwataka Watanzania kuhakikisha wanatumia fedha wanazozipata kwa uangalifu mkubwa, ikiwamo kuzielekeza katika matumizi ya msingi, kwani hali ya sasa imekuwa ngumu tofauti na zamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles