23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makinda ataka mabadiliko sheria ya ndoa

SPIKA Mstaafu, Anna Makinda
SPIKA Mstaafu, Anna Makinda

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

SPIKA Mstaafu, Anna Makinda ameiomba serikali na mamlaka husika kuanza mchakato wa kusukuma mabadiliko ya sheria ya ndoa ili kupanua wigo wa haki za wanawake na watoto nchini.

Akizungumza katika kongamano la kwanza la kitaifa la haki za wanawake, lilioandaliwa na Mfuko wa msaada wa kisheria nchini (LSF) jana jijini Dar es Salaam, Makinda alisema kwamba sheria ya ndoa ya mwaka 1971 imepitwa na wakati na inahitaji marekebisho makubwa ili kutoa haki kwa wanawake nchini.

“Hii sheria ya ndoa inawatenga sana wanawake nchini katika suala la mirathi na haki za mwanamke katika ndoa, na kuacha watoto wengi wakiteseka…ni wakati muafaka sasa kwa wanaharakati kusaidiana na wabunge ili kuleta marekebisho ya hizi sheria kandamizi kwa manufaa ya jamii nzima ya Tanzania” alisema Makinda ambaye ni Spika Mstaafu.

Alisema kwamba marekebisho hayo makubwa au kuandikwa upya kwa sheria ya ndoa itakuwa hatua moja kubwa katika kulinda haki za wanawake za kumiliki mali, kama vile mashamba na kadhalika.

“Nikiwa mbunge, waziri na baadaye spika tulipambana vikali katika kubadilisha sheria ya ardhi ili kuwapa watu wa hali ya chini kupata nafasi ya kumiliki ardhi, sasa na hii sheria ya ndoa inapaswa kushughulikiwa kwa haraka ili kuweza kutoa matokeo chanya kwa jamii,” aliongeza.

Aliomba mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kushirikiana na serikali katika majadiliano hasa katika mambo ya mirathi na ndoa ili kuhakikisha upatikanaji wa marekebisho hayo yanapatikana haraka.

“Ni muhimu pia masuala haya ya haki za wanawake na watoto kufundishwa katika shule za msingi na sekondari ili kupeleka elimu hiyo ya uraia kwa wanafunzi nchini nzima, ila ni muhimu kushirikiana na serikali ili kufanikisha hayo,” aliongeza

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu, Mfuko wa Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk alisema kwamba mfuko lengo lake kuu ni kuongeza haki na usawa kwa wanawake nchini kupitia uwezeshaji wa fedha na mafunzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles