24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

Makamu wa rais wa Zimbabwe apinga kashfa ya ngono dhidi yake

Harare, Zimbabwe

Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Kembo Mohadi, amejitetea kuhusu madai ya kashfa ya kingono inayomkabili kupitia vyombo vya habari.

Amesema yeye ni mwathiriwa wa udukuzi na saiti iliyofanyiwa marekebisho baada ya gazeti moja la mtandaoni kuchapisha rekodi ya mawasiliano yake ya simu na wanawake tofauti wanaodaiwa kumfanyia kazi.

Akiwa amevalia barakoa na sauti yake kutosikika vizuri, kiongozi huo mwenye umri wa miaka 71 aliwaambia waandishi wa habari kwa rekodi hiyo ilifanyiwa ukarabati akisisitiza hakuhusika na madai hayo.

“Mimi sina hatia, ni mwathiriwa wa hila za kisiasa zinazoendeshwa kitapeli,” amesema.

Aliongeza kuwa madai hayo ni ya uongo na yanalenga kumharibia sifa kama kiongozi wa kitaifa.

Msemaji wa serikali ameweka mtandaoni video ya, Mohadi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles