27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yamuachia huru Halima Mdee

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee (Chadema) ameachiwa huru baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuona Jamhuri wameshindwa kuthibitisha mashtaka ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli.

Hukumu imetolewa leo Alhamisi Februari 25, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliyekuwa aliyesikiliza kesi hiyo tangu mwaka 2017.

“Upande wa mashtaka katika kesi hii ulikuwa na mashahidi watatu, baada ya mahakama kupitia ushahidi wao imejiridhisha kwamba upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa bila kuacha shaka yoyote.

“Mahakama inamuona mshtakiwa hana hatia inamuachia huru,” amesema Hakimu Simba.

Mdee alishtakiwa akiwa mbunge wa Kawe kupitia Chadema alikuwa akikabiliwa na shtaka moja la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli.

Alikuwa anadaiwa kusema kuwa Rais Magufuli anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki, kauli zilizodaiwa na upande wa mashtaka kuwa ni za udhalilishaji dhidi ya Rais na kwamba maneno hayo yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Kauli hiyo anadaiwa kuitoa Julai 3, 2017 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa, Kinondoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles