27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Makamba atangazwa mwanasiasa bora kijana

makambaNa Elias Msuya, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Januari Makamba ametajwa kuwa mwanasiasa bora kijana na taasisi ya Tanzania Awards International, jijini Dar es Salaam juzi.
Makamba ameshika nafasi hiyo akiwapita wanasiasa wengine vijana ambao ni pamoja na Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Wabunge Vick Kamata, Esther Bulaya, David Kafulila na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita.
Katika tuzo za mwanasiasa mtu mzima ushindi umechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na
Katika kundi hilo, Profesa Muhongo alishindanishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, Waziri Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose Migiro na Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu.
Wengine ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula.
Tuzo ya jamii ilichukuliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Waliopewa tuzo za heshima katika jamii ni Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere na Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela.
Si Makamba, Profesa Muhongo wala Mengi waliohudhuria shughuli hiyo badala yake waliwakilishwa na ndugu zao.
Hata hivyo sherehe za kutoa tuzo hizo zilidororora hasa kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliyepangwa kuwa mgeni rasmi hakuhudhuria na aliwakilishwa na mkuu wa mkoa lakini naye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Akitoa ufafanuzi wa tuzo hizo, Mratibu wa Taasisi hiyo, Amani Mwaipaja alisema zilikuwa katika vipengele vitano ambavyo ni tuzo ya jamii 2015, tuzo za jamii ya heshima, tuzo jamii katika haki za binadamu, tuzo ya mwanasiasa kijana na tuzo ya mwanasiasa mzee.
“Tumeangalia vigezo kadhaa ikiwa pamoja na uadilidu, uaminifu, utii katika sheria, kuwa na maono, mikakati na mipango,” alisema Mwaipaja.
Kuhusu mchakato uliotumika kuwapata washindi, Mwaipaja alisema ulikuwa shirikishi ukihusisha mitandao ya Jamii kama vile Facebook, Tweeter, Instagram na Jamii Forums.
“Baada ya kupata mapendekezo tulichambua majina 13 ya mwanasiasa mtu mzima na majina mengine 13 ya mwanasiasa kijana. Asilimia 70 ya kura zilitokana na mapendekezo ya wananchi na asilimia 30 zilitokana na kamati ya tuzo chini ya mwenyekiti DJ Maregesi,” alisema Mwaipaja.
Akizungumzia tuzo hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii na kutenda haki kwa jamii.
“Katika dunia hii, jambo lolote unalofanya iwe ni kuzalisha mali au kutumia unachozalisha, lazima utumie kanuni ya haki kwa jamii,” alisema Mushi.
Hata hivyo, alisema changamoto kubwa inayoikumba nchi kwa sasa ni mauaji ya albino jambo linalopaswa kupigwa vita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles