25.4 C
Dar es Salaam
Thursday, January 9, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MAKAKALA: OLE WENU MNAOHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU

NA HADIJA OMARY


KAMISHINA Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, amekemea vikali tabia ya wananchi kushiriki aidha kwa kuwahifadhi au kuwasafirisha wahamiaji haramu kwa njia za panya.

Amesema kwa yeyote atakayebainika kushiriki kwenye vitendo hivyo, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Dk. Makakala alitoa kauli hiyo juzi, mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili aliyoifanya mkoani Lindi, ambako alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa idara yake katika Wilaya za Kilwa, Nachingwea, Lindi na Ruangwa.

“Ipo tabia ya baadhi ya Watanzania kushirikishwa katika biashara hiyo haramu ya kuwasafirisha ama kuwahifadhi wahamiaji, hasa kwa maeneo yaliyo mipakani mwa nchi,  nawaomba waache mara moja.

“Sheria ya Uhamiaji kwa sasa imeongezewa makali, mtu atakayejihusisha na shughuli hiyo basi atatozwa faini isiyopungua Sh milioni 20, kifungo cha miaka 20 au vyote kwa pamoja, ikiwamo kutaifisha mali zote zitakazohusika kuwasafirisha wahamiaji hao,” alisema Dk. Makakala.

Awali akisoma taarifa ya utendaji kazi ya uhamiaji kwa Mkoa wa Lindi, Ofisa Uhamiaji Mkoa huo,  Abdallah Katimba, alisema kutokana na doria zinazofanywa  mara kwa mara katika nyumba za kulala wageni, vituo vya mabasi, barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Mtwara na njia za michepuko, wameweza  kukamata raia wawili wa Vietnam, watano wa Ethiopia na mmoja wa Malawi.

Katimba aliongeza kwamba, kuwapo kwa Mkoa wa Lindi katika mwambao wa Bahari ya Hindi kumesababisha raia wengi wa Msumbiji  kulowea nchini kutokana na shughuli za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Alisema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika utoaji wa vitambulisho vya Taifa, wamebaini watu 8,123 si raia wa Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles