22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

AMINA MWIDAU: ANAYEMPINGA MAGUFULI NI MPINGA MAENDELEO

Na susan Uhinga, Tanga


Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), amesema mtu yeyote anayepinga juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais John Magufuli ni mpinga maendeleo na hafai kuwa miongoni mwa Watanzania wapenda maendeleo.

Aidha, amesema ameamua kujiunga na CCM ili kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli.

Mwidau ameyasema hayo katika Viwanja vya Makorora wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makorora.

“Nilipokuwa mbunge nikiwa bungeni pale Dodoma, tuliomba kwa Mwenyezi Mungu atupe kiongozi atakaeiongoza Tanzania awe mchapa kazi na mzalendo. Na hili naliona kwa Rais Magufuli, hivyo sasa ni wakati wangu wa kumuunga mkono,” amesema.

Wakati huo huo, mgombea udiwani wa Kata ya Makorora, Omari Mzee ambaye alikuwa Diwani wa CUF amerudisha kadi ya chama hicho na kuomba wananchi wa kata hiyo kumchagua ili aweze kuwaletea maendeleo akiwa ndani ya CCM ambapo anaamini ataweza kutekeleza ahadi zake kwa wapiga kura.

“Ndugu zangu Wanamakorora miye ni mzaliwa wa hapa hivyo nichagueni miye kwa maendeleo ya kata hii, huko nyuma nilipotoka kwa kwenda upinzani chama chenye migogoro hivyo hakukuwa na fursa ya kutekeleza ahadi za maendeleo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles