26 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAJENGO YA WACHINA KUGEUZWA HOSPITALI

Na IBRAHIM YASSIN, TUNDUMA

MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba mkoani Songwe, wamekubaliana kubadilisha matumizi ya majengo yaliyokuwa kambi ya Wachina waliokuwa wakijenga barabara ili yawe hospitali ya wilaya hiyo.

Akizungumza hivi karibuni kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Ally Mwafongo, alisema wamekubaliana kuchukua majengo hayo kwa kuwa yatawasaidia kuwa na hospitali kwa urahisi.

“Mji wa Tunduma umekuwa ukikua siku hadi siku na shughuli za kijamii zinazidi kuongezeka sambamba na idadi ya watu kuongezeka.

“Kutokana na mabadiliko hayo, hata kituo cha afya tulichonacho kimekuwa kikizidiwa na wagonjwa. Kwa hiyo, tumeona majengo hayo yakitumika kama hospitali ya wilaya, yatasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika kituo hicho.

“Ieleweke kwamba, uamuzi wa kubadili matumizi ya majengo ya kambi hiyo na kuwa hospitali ya wilaya, hakumaanishi kuwa kituo cha afya kitakufa,” alisema Mwafongo.

Naye Herode Jivava ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, alisema uamuzi wa kuyachukua majengo hayo ulitokana na kituo cha afya za Tunduma kuzidiwa na idadi kubwa ya wagonjwa.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Chiwezi, Francis Sikanyika, alisema wakati uamuzi huo ukifanyika, lazima halmashauri ya mji huo ijenge dampo katika eneo la Namole ili kupunguza uchafu mjini Tunduma.

Akizungumzia uamuzi wa kuchukua majengo hayo, Katibu Tawala, Mkoa wa Songwe, Elia Ntandu, alisema Serikali ya mkoa huo imepitisha uamuzi huo kwa kuwa inajua umuhimu wake.

Kuhusu kuzagaa kwa taka, alisema Halmashauri ya Mji wa Tunduma, inatakiwa kukagua maeneo yote ya makazi na shughuli za kijamii na kuangalia namna ya kukabiliana na uchafu huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles