28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa viwanda vya wazawa Vitapunguza tatizo la ajira

Yohana Paul Na Sheila Katikula -Mwanza

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa, amesema ongezeko la idadi ya Watanzania wanaowekeza sekta ya viwanda, ndiyo suluhu ya kudumu ya tatizo la ajira ambalo linazidi kukua kila kukicha.

Aliyasema hayo juzi jijini  Mwanza, wakati akifungua sehemu mpya ya uwekezaji  na upanuzi wa kiwanda cha Nyanza Bottling Company kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji mbalimbali.

Alisema Serikali inatambua uwapo wa tatizo la ajira,ni vigumu na siyo rahisi wasomi wote kuajiliwa serikalini.

Alisema ndiyo maana, imekuja na mkakati mpya wa sera ya viwanda kwani vina mchango mkubwa punguza tatizo hilo.

“Tatizo la ajira linaloonekana, siyo jipya na wala halipo Tanzania pekee, bali lipo dunia nzima, nchi nyingi ambazo tayari zimefanikiwa kuondokana na changamoto ya uhaba wa ajira zilitoa  kipaumbele cha uwekezaji  sekta ya viwanda kama inavyofanya Serikali.

“Tunaamini katika uchumi wa viwanda kama suluhu ya tatizo la ajira, lazima tuelewe mwarobaini kamili wa tatizo hili, utakuja pale viwanda vingi vitamilikiwa na wazawa.

“Natoe rai kwa wazawa na wageni wenye viwanda kuhakikisha wanatoa fursa ya ajira kwa Watanzania kama inavyofanya kampuni ya Nyanza, tuachane na kasumba ya kuwapa kipaumbele wageni kwa kigezo cha taaluma na uzoefu, niwahakikishie vyuo vyetu vinatoa vijana waliokamilika ambao mkiwatumia taifa litafaidika na tutaondoa malalamiko ya tatizo la ajira,” alisema Majaliwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyanza Bottling company, Mwita Gachuma alisema kutokana na sera nzuri ya viwanda,kampuni yake imefanikiwa kuwa na mwendelezo mzuri wa uzalishaji kanda ya ziwa na maeneo ya jirani.

Alisema maendeleo mazuri ya kiwanda hicho, yameiwezesha kampuni anayoisimamia kutoa ajira kwa vijana wengi na kulipa kodi ya Serikali, bila kikwazo  hivyo kuchangia kuinua uchumi wa taifa.

“Mafanikio hyametufanya kuweza  kulipa kodi serikalini shilingi bilioni 54.6 kwa miaka mitano, tumetoa ajira rasmi 1,600, zisizo rasmi 3,500 kwa watu ambao tunawapatia malipo yao bila kukwama.

“Niihakikishie Serikali uwekezaji mpya uliozinduliwa na waziri mkuu, utaongeza fursa za kiuchumi kwa vijana wetu, utasaidia kuchangia kuinua pato la taifa,”alisema.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Innocent Bashungwa alisema ni wakati muafaka Watanzania kutumia fursa ya maendeleo ya miundombinu hasa ujenzi wa reli ya kisasa, maboresho katika usafiri wa anga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles