30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa dini wataka Serikali kugharamia bima

Ramadhan Hassan- Dodoma

VIONGOZI  wa  dini wameishauri Serikali kugharamia gharama za bima ya afya kwa kila Mtanzania  ili apate matibabu ya uhakika pindi anapoumwa.

Hayo yalielezwa jijini hapa jana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Canon  Matonya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti iliyotolewa na Kamati ya  Viongozi wa Dini kuhusu bima ya afya iliyoboreshwa (CHF).

Matonya ambaye ni Katibu Mwenza wa Kamati hiyo, alisema suala la bima la afya bado ni changamoto kubwa kutokana na watu wengi kutokuwa na bima.

Alisema kutokana na hali hiyo, ni vyema Serikali ikajitahidi kila Mtanzania awe na bima hiyo ili anapoumwa aweze kwenda hospitali haraka,ugonjwa haupigi hodi.

Alisema kutokana na utafiti walioufanya kwa muda wa mmoja, wamebaini  mambo mbalimbali, ikiwamo wastani wa uchangiaji sekta ya afya umeonyesha Serikali inachangia asilimia 35,wadau wa maendeleo asilimia 37 na watoa huduma binafsi asilimia 28, jambo linaloonyesha utegemezi mkubwa katika vyanzo vya nje vya bajeti

Naye Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Kasusu Mvumbo alisema afya ni suala muhimu kwa mwanadamu yoyote, wao viongozi wa dini wana jukumu kubwa kuhamasisha waumini kujiunga na bima ya afya iliyoboreshwa

Mratibu wa CHF kutoka Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk.Boniface Richard alisema Serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afya kwa wananchi na bima ya CHF, iliyoboreshwa  imeboreshwa zaidi kwa kupanua wigo wa matibabu kwa mchangiaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles