27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: SEKOMU kamilisheni mahitaji ya TCU

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki inayomiliki Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) ukamilishe mahitaji ambayo yataiwezesha Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kukiruhusu chuo hicho kuendelea na udahili.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Januari 16, 2021) wakati alipokutana Askofu Mteule wa Dayosisi hiyo Mchungaji, Dk. Msafiri Mbilu pamoja na viongozi wengine wapya waliochaguliwa. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya Askofu Dk. Mbilu kuiomba Serikali iusaidie uongozi wa Dayosisi hiyo katika kukiwezesha chuo hicho kufunguliwa na kuruhusiwa kufanya udahili.

Mwaka 2018 TCU ilikisitishia chuo hicho kufanya masomo na udahili wa wanafunzi katika ngazi zote za masomo baada ya kukosa vigezo.

“Kamilisheni mahitaji yatakayokifanya chuo chenu kiweze kuendelea kufanya udahili. Taarifa niliyonayo ni kwamba TCU walishakuja kukutana nanyi na kufanya ukaguzi, walitoa mahitaji kadhaa ambayo mnapaswa kuyakamilisha na nimesikia mmeridhia na kazi hiyo inaendelea,” amesema.

Mbali na maagizo hayo, pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi wa dini nchini kutokana na mchango mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa Taifa. “Viongozi wa dini ni watu muhimu sana, nchi imetulia na ina amani, hivyo kuwa kimbilio kwa waliokosa amani makwao.”

Awali, Askofu Dkt. Mbilu alimweleza Waziri Mkuu kwamba Chuo Kikuu cha SEKOMU kimezuiliwa kufanya udahili kutokana na changamoto mbalimbali za kimfumo wa ndani ya Dayosisi na ndani ya chuo ikiwa ni pamoja na kuwa na viongozi wa kukaimu kwa muda mrefu jambo ambalo kwa sasa tayari limeshapatiwa ufumbuzi.

Ametaja changamoto nyingine kuwa ni madeni makubwa yakiwemo ya mishahara ya watumishi, ambapo tayari uongozi umeshaanza kulipa malimbikizo hayo na  wameweka mipango ya kumaliza kulipa madeni hayo. Pia, kiongozi huyo alisema chuo kimeshapata waalimu wa kutosha kwa ajili ya kufundisha wanafunzi mara kitakapofunguliwa.

Askofu Dk. Mbilu amesema kabla ya kufungiwa Chuo Kikuu cha SEKOMU kilikuwa kinatoa elimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu maalumu ya kuwahudumia watu wenye ulemavu katika ngazi ya shahada na shahada ya uzamili, hivyo kimetoa wataalamu wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles