32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Acheni kujipendekeza kwa viongozi- James

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-
CCM) Taifa, Kheri James amewataka vijana kusimamia sera bora inayolenga kuleta Maendeleo kwa Watanzania wote na kucha kujipendekeza kwa viongozi.

James ameyasema hayo leo, Januari 16, wakati wa uzinduzi wa mradi wa nyumba ya mtumishi wa (UV-CCM) Mkoa wa Kilimanjaro iliyojengwa kwa nguvu za vijana.

Amesema wapo baadhi ya vijana wamekuwa wakijipendekeza kwa viongozi wa serikali lakini hawana hata uwezo, hivyo kuwataka vijana hao kuendelea kufanya kazi kwani watapimwa kwa utendaji kazi wao.

“Hatutengemei viongozi waliopewa dhamana ya uongozi kwenda kufanya kazi ambazo wananchi hawakuwatuma, hakikisheni mnatatua kero zao kwa wakati, fanyeni kazi acheni kujipendekeza kwa viongizi,” amesema James.

Aidha, James amewataka vijana kujenga utamaduni wa kuwa na fikra mpya na wabunifu ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kisiasa.

“Hakikisheni mnakuwa sehemu ya kuishauri serikali katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuleta ufanisi wa kazi,”amesema.

“Nendeni kwa wananchi mkawe wakalimani wa sheria zinazopitishwa na serikali ili wananchi wawe na uelewa juu ya sheri dogo dogo, mkifanya hivyo mtakuwa mmekisaidia chama,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles